Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
- Thread starter
- #21
Kuandika kila mtu anaweza. . . . huko mtaani mnawaambia? Au mnaishia kucheka cheka na kusifia?
Ya mitaani bora tuwaachie maana itaonekana kuingilia uhuru wa mtu binafsi. Jamii zina njia nyingi tu za kukosoa, kuonya na kutahadharisha kupitia njia mbalimbali tangu historia ya mababu zetu.
Katika tamaduni mbalimbali kumekuwa na ngoma za asili, na ukigundua nyimbo zao zilikuwa za kukosoa, kumsema fulani aliyetenda jambo ambalo si la wakaida iwe zuri au baya. Tathmini ya kizazi cha leo ni zaidi ya muziki pia kuna vyombo vya habari kama magazeti, TV na radio ambavyo hutoa michango mikubwa katika kujenga jamii.
Wananchi wenyewe wana nafasi ya kujifunza kutokana na vyombo mbalimbali vinavyousia, wasanii mbalimbali wanavyoonya na kushauri, si kusubiri mpaka mtu akunyoshee kidole kuonyesha upungufu wa kutokuwa na hulka ya kujitambua.
Nakumbuka wiki hii kuna picha fulani ya msanii wa taarabu kutoka kule Zenj alivyoshambuliwa pale jukwaa la picha, ingawa naweza kumjengea utetezi wa kwamba alikuwa na maana ya kuwa mzuka jukwaani kurusha juu juu mioyo ya wapenzi wake wa muziki, lakini ujumbe wa wengi wasivyopendezwa na too much make up ile anaweza kujifunza na kufanya masahihisho kupunguza kilichozidi aonekane kama kavaa mask.