Make up na mask (kifuniko cha uso) kuna tofauti gani?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

1. Mchawi anapokujia usiku, akijua wewe u Roho, utamwona,hupaka unga usoni kisha hunuiza maneno Fulani Fulani Ili asionekane, na nuizo Hilo huambatana na kufunika sura yake Kwa kifuniko Cha mnyama kama mbwa au paka, nyoka, ngombe nk nk.

Ndio maana utaota ukikimbizwa na nyoka au mbwa,ngombe, Si n'gombe wale, ni watu waliofunika NYUSO zao Kwa kunuiza maneno Fulani Fulani Ili usiwaone/ wasionekane.

Mtu wa Giza akitaka uharikikiwe, atakufunika kifuniko Cha uso( mask usoni) au kukuwekea uso fake wa bibi kizee au kinyago Cha kutisha Ili Kila akuonaye akuchukie asikutizame Ili uharibikiwe. Sasa kwann nawe uufunike utukufu wako(uso) Kwa make up /vifuniko vya uso?

2. Mwizi / Jambazi anayejua anafahamika na asingependa kuonekana, atavaa mask( kifuniko Cha uso Ili asijulikane. Likewise, wasiojulikana huvaa mizola, miwani ,wigs nk nk Ili wasitambulike.

3. Kahaba akijua kuwa anataka kuwahadaa wanunuzi, hununua vipodozi vya Kila aina Ili kuhakikisha anafunika uso wake Kwa kutengeneza mwonekano wa kitu kingine kisichofanana na Yeye halisi, na mwonekano huo mpya ndio Hasa silaha ya kuwafunga NAFSI wanunuzi kuingia kwenye mtego huo wa kahaba, na Kwa kuwa kahaba ni shimo refu, yeyote aingiaye humo, hatotoka kamwe, lakini chanzo Cha yote ni makeup, kifuniko Cha uso.

SWALI KWA WALIOOLEWA( WAKE ZA WATU) NA WANA WA MUNGU.

Hizi make up ni za nini?

Kwanini kubadili au kuficha sura Yako Kwa kuvaa sura ingine, Ili iweje?

NB; Jambazi, mchawi na kahaba ni watoto wa baba mmoja, na hufanya KAZI Kwa ushirika wa karibu sana ingawa Kwa nje ni kama maadui.

Ikiwa ungependa kuingia katika familia ya Mungu, fuatisha Sala hii:

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, UZINZI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

Karibuni 🙏
 
1 Waraka wa kwanza wa Yohana 2:15-17)

15: Msiipende Dunia, Wala mambo yaliyomo katika Dunia.

Mtu akiipenda Dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16: Maana Kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili,tamaa ya macho, kiburi Cha Uzima, havitokani na baba, Bali vya Tokana na Dunia.

17. Na Dunia inapita pamoja na tamaa zake, Bali Yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
 
Salaam, Shalom!!

1. Mchawi anapokujia usiku, akijua wewe u Roho, utamwona, hunuiza maneno Fulani Fulani Ili asionekane, na nuizo Hilo huambatana na kufunika sura yake Kwa kifuniko Cha mnyama kama mbwa au paka, nyoka, ngombe nk nk.

Ndio maana utaota ukikimbizwa na nyoka au mbwa au ngombe, Si ngombe wale, ni watu waliofunika NYUSO zao Kwa kunuiza maneno Fulani Ili wasionekane.

2. Mwizi / Jambazi anayejua anafahamika na asingependa kuonekana, atavaa mask( kifuniko Cha uso Ili asijulikane. Likewise, wasiojulikana huvaa mizola, miwani ,wigs nk nk Ili wasitambulike.

3. Kahaba akijua kuwa anataka kuwahadaa wanunuzi, hununua vipodozi vya Kila aina Ili kuhakikisha anafunika uso wake Kwa kutengeneza mwonekano wa kitu kingine kisichofanana na Yeye halisi, na mwonekano huo mpya ndio Hasa silaha ya kuwafunga NAFSI wanunuzi kuingia kwenye mtego huo wa kahaba, na Kwa kuwa kahaba ni shimo refu, yeyote aingiaye humo, hatotoka kamwe, lakini chanzo Cha yote ni makeup, kifuniko Cha uso.

SWALI KWA WALIOOLEWA( WAKE ZA WATU) NA WANA WA MUNGU.

Hizi make up ni za nini?

Kwanini kubadili au kuficha sura Yako Kwa kuvaa sura ingine, Ili iweje?

NB; Jambazi, mchawi na kahaba ni watoto wa baba mmoja, na hufanya KAZI Kwa ushirika wa karibu sana ingawa Kwa nje ni kama maadui.

Ikiwa ungependa kuingia katika familia ya Mungu, fuatisha Sala hii:

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, UZINZI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

Karibuni 🙏
Nilivosoma kichwa cha thread si nikajua ni mambo ya vipodozi.
 
2025 ni mwaka wa kuwa mpya....

Ni muda wa kwenda sawa na MUNGU wangu.

Haya ya ulimwengu tuyaache tu mkuu, nimeyaishi mpaka sasa sijaona faida yake kubwa.

TO GOD BE THE GLORY 🙏
 
Amen,

Ubarikiwe 🙏
 
Kazi ya Mask ni kudanganya ili ukweli usijulikane.
Biblia haizungumzii hizi Makeup💄 wanazopaka wadada, Kuna Mask inayofunika Ufahamu hiyo ndio inapoteza wengi.

2 Wakorintho 3:13-15 TKU
[13] Hatuko kama Musa, ambaye alifunika uso wake ili watu wa Israeli wasiendelee kuona kuwa utaratibu wa zamani wa kumtumikia Mungu ulikuwa unaelekea mwisho. [14] Lakini mioyo yao ilikuwa imefungwa. Na hata leo, watu wale wanapolisoma agano la kale, fahamu zao zinakuwa zimefunikwa. Ni kwa kupitia Yesu Kristo tu agano la kale linaondolewa. [15] Ndiyo, hata leo, wanaposoma sheria ya Musa, fahamu zao zimefunikwa.
 
Soma (Isaya 3:16-25)
 
Vifuniko vya uso vimelenga kuondoa utukufu wa mtu ambao ni Nuru usoni, kibali Kwa Kila akuonaye kikufungulie milango ya baraka.

Kufunika uso Kwa masks( vifuniko vya uso) kama makeups ni kujiletea nuksi.

Wana wa Mungu, tuache mambo hayo.
 
Hizo Makeup unazozungumzia ni sawa na Kupaka mafuta tu. Hata wewe upo mlemle kupaka mafuta usoni ni kubadilisha uhalisia wako
 
Soma (Isaya 3:16-25)
Mkuu hata Bible huwa huelewi kumbe.

Hapo Isaya alikuwa hazungumzii wanawake wasayuni, alikuwa analizungumza Taifa la Israel.

Hayo yote yaliyosemwani Kiburi cha wana wa Israel kujiona ni Bora kuliko wengine.
Kiburi hicho kilisababisha kuvunja Agano lao na Mungu.

Hivyo Hasira ya Mungu ilikuwa juu yao.

Kwahiyo ndugu Rabbon hapo(Isa 3:16-) hawaongelewi wanawake unaowajua
 
Unajua Kila neno ulisomalo ndani ya BIBLIA Lina tafsiri Saba, na WANADAMU tumepewa kujua tafsiri Moja Hadi tatu pekee, zilizobaki ni Siri za Mungu?

Ndio maana mstari mmoja, wahubiri 100 wanaweza pata Kila Mmoja tafsiri ya kusaidia katika angle mbalimbali?

Kwanini unaamua kubaki na tafsiri Moja pekee, au ndio uwezo wako ulipoishia kuyajua maandiko?

Nenda pale Israel uliza ikiwa wanawake wa kiyahudi wanaruhusiwa kutoga na kuvaa Pete za masikioni,

Ikiwa wao walikatazwa tangu enzi na enzi Kwa sababu za kiroho, Kanisa la Leo wamepata wapi ruksa ya kujifananisha na Dunia na kutukana uumbaji wa Mungu?
 
Hebu toa aya Inayosema wana wa Israel walizuiwa kuvaa hereni
 
Mimi ninayo maandiko,

Wewe leta andiko lililoruhusu wanawake kuvaa mawigi, kutoboa pia, kupaka udongo wa makeup usoni, kufuga kucha wawe kama misukule, kuvaa suruali, nguo za kubana nk nk
 
You wake up, put makeup on, stare in the mirror, but it's clear that you can't face what's wrong.
No need to fix what God already put his paint brush on.-J .Cole . 'Crooked Smile'
 
Unajua Kila neno ulisomalo ndani ya BIBLIA Lina tafsiri Saba, na WANADAMU tumepewa kujua tafsiri Moja Hadi tatu pekee, zilizobaki ni Siri za Mungu?

Ndio maana mstari mmoja, wahubiri 100 wanaweza pata Kila Mmoja tafsiri ya kusaidia katika angle mbalimbali?
Ok
Kwanini unaamua kubaki na tafsiri Moja pekee, au ndio uwezo wako ulipoishia kuyajua maandiko?

Nenda pale Israel uliza ikiwa wanawake wa kiyahudi wanaruhusiwa kutoga na kuvaa Pete za masikioni,

Ikiwa wao walikatazwa tangu enzi na enzi Kwa sababu za kiroho, Kanisa la Leo wamepata wapi ruksa ya kujifananisha na Dunia na kutukana uumbaji wa Mungu?
Mkuu...
Kupitia hapa Mungu mwenyewe ndiye aliyewapamba tukiamua kufuata namna yako ya kutafsiri Bible

Eze 16:10-13 SUV
[10] nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri. [11] Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako. [12] Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako. [13] Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme.
 
Mimi ninayo maandiko,

Wewe leta andiko lililoruhusu wanawake kuvaa mawigi, kutoboa pia, kupaka udongo wa makeup usoni, kufuga kucha wawe kama misukule, kuvaa suruali, nguo za kubana nk nk
Wewe unaweza kuleta maandiko yanakuambia uamke Uoge asubuhi kisha upake mafuta mwili wako.

Kwanini unapaka mafuta ya mgando usoni?
 
Mkuu...
Kupitia hapa Mungu mwenyewe ndiye aliyewapamba tukiamua kufuata namna yako ya kutafsiri Bible

Eze 16:10-13 SUV
[10] nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri. [11] Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako. [12] Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako. [13] Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme.
Sasa endelea mistari ya mbele,

Mapambo hayo ndio yamemfanya kujiinua, na kufanya uzinzi, ukahaba na Ibada ya sanamu.

Ukimruhusu mkeo kuvaa vimini na nguo za kubana, matokeo ni hasi.
 
Back
Top Bottom