Makengeza huitwaje kwa Kiingereza?

Makengeza huitwaje kwa Kiingereza?

mkuu kama anakutega kimapenzi neno seduce nahisi linafaa...ila kwa muktadha wa polisi au huo wa mabeki neno tega linaweza kuwa trap au plot .....baada ya kusema hayo mimi nilikuwa nauliza neno "kigugumizi" kwa kiingereza ni nn?

hili naona pia kama linafaa trick
 
Fikiria zaidi ya hapo ulipofikiria...sio kwamba dictionary hakuna...ishu ni context ya neno...

kwani context ya neno huwezi kuipata kwenye dictionary (kamusi)? maana huwa zinakuwepo options za maana zaidi ya moja.
 
Kigugumizi ni "stutter." Unaweza kulicheki zaidi online kuna maelezo mazuri.

Kuhusu "kutega," nililifikiria hilo neno "trap," ahsante sana, lakini nikakwama mahala. Tatizo la trap ni kwamba, ukisema "the police trapped the thief" inamaanisha wamemkamata mtegoni tayari. Mimi nataka kabla hawajambaka mtegoni, wamemtega tu. Ndo hapo "trap" inapogomba.

Trick! Iwe ni katika kujipanga kukamata mwizi au uwanjani kwenye mpira kama ulivyofafanua kwenye maelezo yako ya awali! Ni maoni yangu tu.
 
Asanteni sana wadau....nilikuwa mbali kidogo
 
Na take macho km mtu kala kungu, yanaitwaje?
 
Back
Top Bottom