Makinda alimkatalia Mnyika, Leo hii Jaji Mkuu analalamika

Shida kubwa ya hao watu wanaoitwa CCM wao wanashabikia kila kinacholetwa mbele yao na mkubwa wao, hawana muda wa kukiangalia wala kukitafakari wao wanachojua ni kumzodoa anayetafakari na kuhoji
 
Nini kimeipata mahakama mpaka hawaitaki tena hiyo sheria?
 
Duh sikujua tuna sheria ya kipumbavu kama hii, kweli kwa akili hizi ni wazi umaskini wetu ni kwa sababu tunaongozwa na wasio na akili
Akili za kuiba rasilimali za Tanganyika, kuuwa, na kujimilikisha madaraka kwa familia zao wanazo sana.

Ila akili ya kuibadili Tanganyika kuwa dude kubwa la maendeleo kama UK, USA, China, wamegoma makusudi, na hawatakaa walete maendeleo,

Sababu siku wakiamua kutunga sheria makini watakoma kuiba na hawana Mpango wa kuacha ushetani.
 
Miswaada inaandikwa kwa lugha ya kisheria ambayo ni ngumu kidogo, sasa unafikiri mtu kama babalevo ataelewa nini. Ndio maana mfumo hauwataki watu kama Lissu bungeni
Upo sahihi hao wanaoandika hiyo miswaada si Wanasheria kwa nini wanapeleka vitu vya hovyo hovyo Kila kukicha..
 
Hadi Inakera... Mnyika alijitahidi kuwaelewesha lakini wapi... CCM wakiwa na jambo lao hata kama ni la kijinga watalishadadia mpaka utashangaa.
Kuna siku moja walikuwa wanampina Lissu kwa kuwa yupo Upinzani ila alikua anawatetea wao nadhani walikuja kufuta ile sheria tena hao jamaa huwa siwaelewi kabisa wanataka nini..
 
Hakuna adui mbaya nchi hii kama CCM, iwe kwa maendeleo, haki au demokradia, CCM.ndiyo kikwazo kikuu. Na tatizo kubwa lianaanzia kwa aina ya watu wanaoongoza CCM. Akili ndogo ndani ya CCM ni sifa kuu ya kupata uongozi.
 
Ndio maana mimi siku zoote hua napigia kura Wabunge wa Upinzani.

Yaani hata leo CHADEMA wakishika nchi, Lazima ntapigia kura Wabunge wa CCM ili kuwe na alternative voice.

Kazi ya Bunge ni kuisimamia serikali, Wabunge wa chama tawala hawawezi kuoinga jambo lililo pitishwa kwenye secretariat za vyama vyao
 
Ukiulizwa kubadili sheria shilingi ngapi, kiasi hili litutie umaskini, utakuwa na majibu? Haya mambo yatajiseti. Hakuna haja ya kujitafutia msongo wa mawazo.
Umeongea kwa matani au unakusudia kuwa tutunge sheria mbovu then tusubiri ijiseti baadae? Kwa umri wako bado ujajua hasara itokanayo na sheria mbovu?
 
Ukiulizwa kubadili sheria shilingi ngapi, kiasi hili litutie umaskini, utakuwa na majibu?
Wabunge waliolipwa kwa kikao hicho kilichoketi mpaka usiku walilipwa kwa tija gani?

Umaskini unatokana na Sheria wanazotunga. Umaskini wa Tanzania umo kwenye Sheria za hovyo zinazotungwa bila ya kuzingatia maslahi ya Taifa.
 
Watanzania tunaongozwa na wapumbavu ujinga hautakwisha bongo, na maendeleo halisia hayawezi kupatikana huku wajinga wakiongoza werevu, vitabu vinasema soma! Vyote Bible na Quran Jambo la kwanza usome kwanza na sifa ya kusoma sio kusoma makaratasi soma, soma someni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…