Tuache visingizio. Kijana yeyote awe msomi au la anatakiwa ajishughulishe, awe tayari kufanya kazi yoyote. Kitu kinachosumbua vijana wasomi ni jinsi jamii inavyowatazama na kuwahukumu. Kusimama majukwani na kuwabeza wasomi ni kuwaongezea msongo wa mawazo. Kwa mtazamo chanya Makinda anataka vijana wasomi wasibweteke- siku hizi ni vijana wachache sana wanapata kazi inayoendana na kozi waliyosomea. Wajitume zaidi, wahangaike mitaani- wajifunze mambo mapya ili kujipatia kipato- si rahisi, lakini msemo wa kiswahili wa penye nia pana njia mara nyingi unafanikiwa. Kazi yoyote itakuongezea "networking "- utafahamiana na watu wengi kuliko kukaa nyumbani.