Makinikeni na hawa matapeli

Makinikeni na hawa matapeli

Juzi kuna jamaangu aliona TV 50” inauzwa 550,000 zanzibar,
Alishawishika sana na kuniuliza kama akiagiza itafika salama,nilimcheka sana na nikamwambia kama usingekutana na mimi ungekua unalia wakati huu
Hao watu wanatumia kigezo cha wao kuwa mbali ili tu utume pesa
 
Watu wamelizwa sana huko visiwani
 
BEI 420,000/=

TUNAJUA MAFUTA YAMEPANDA BEI PIGA CHINI GHARAMA HIZO TUKUPATIE BASKELI YA KISASA YA UMEME YENYE BATTERY [emoji367] YENYE NGUVU KUBWA ZAIDI , UTAWEZA KUTEMBELEA HADI KILOMETER 120-150 BILA KUSUMBUKA / UNAWEZA KUTUMIA MIFUMO YOTE KWA KUKANYAGA PEDAL AU KUENDESHA KWA UMEME TUPIGIE [emoji3513]LEO TUKUHUDUMIE AU TUMA UJUMBE KWA NJIA YA WHATSAPP NO 0755837542/ OFFER YA USAFIRI [emoji924]
BURE NA VIFAA VYAKE BADO ZIPO KARIBU / TUNASAFIRISHA POPOTE TANZANIA NA NJE YA NCHI PIA
LOCATION [emoji625]ZANZIBAR PEMBA KIUYU

========

Ofisini kwetu tuliziona hizo baiskeli na kuvutiwa nazo sana lakini tukaweka mashaka makubwa kwenye bei.. Hivyo kujiridhisha tukafanya mawasiliano na wahusika. Wakasema imebaki moja tuu na tufanye malipo haraka tutumiwe mzigo

Tulicheki na vyanzo vyetu Zanzibar na Pemba lakini tukakuta hakuna kitu kama hicho, tulitumia pia namba tofauti tatu lakini kila moja ilipewa maelezo tofauti

Huko FM/META bado jamaa wanapost na pengine wameshawapiga watu. Nimeleta hapa kama tahadhari ili vilio visije kuwa vingi baadae

View attachment 2302880
Tafadhali.....Kaka mshana naomba kuwasilisha jambo kwako DM au Njia nyingine naweza kukupata....nipo Kilimanjaro....
 
Online business kwa Tanzania,bado sana! Wewe agiza tu,biriani sasa hivi hapo ulipo,utaletewa tofauti na ulivyoagiza au utaletewa muda wanaotaka wao,au isipate kabisa
 
Online business kwa Tanzania,bado sana! Wewe agiza tu,biriani sasa hivi hapo ulipo,utaletewa tofauti na ulivyoagiza au utaletewa muda wanaotaka wao,au isipate kabisa
Inaharibiwa na wachache wasioijua na wachache wenye nia ovu

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom