Makocha kumi bora kuwahi kufundisha mpira wa miguu Tanzania 1990-2022

Sianga iliwaletea sifa makolo ila alipougua hawakufanya mchango wowote na kumtembelea kunfariji ili kutambua mchango wake kwa timu hiyo
 
Unaandika orodha bila kusema mafanikio ya kila kocha, hii ni takataka
 
Kwahiyo mnaposema kuwa simba ni kubwa afrika kumbe mnajitoa akili huku munajua wazi ukubwa wa timu ni kuchukua vikombe na sio kushiriki
CAF wanatumia point kuweka ranking ya timu na hizo zinaonesha Simba ni timu kubwa.
 
Hizi ni porojo za vijiweni. Maximo ana mafanikio gani hapa Tanzania? Taja vikombe alivyobeba uache blah blah.

Au taja mchezaji yeyote aliyeibuliwa na kufanywa bora na maximo.
We jamaa bna!!..hivi uliiona stars ya msola iliyocheza na rwanda maximo akiwa jukwaani pale uhuru!!?..ilikua uharo tu,pasi nne shida, peleka miaka mbele itazame stars iliyocheza na Cameroon ya etoo 2008 pale kwa mkapa..bila maximo nizar,shindika,babi,kigi,nyoni nk usingewajua
 
Sianga iliwaletea sifa makolo ila alipougua hawakufanya mchango wowote na kumtembelea kunfariji ili kutambua mchango wake kwa timu hiyo
Sianga alisema walikua wakinunua mechi za ligi na mo...na ugomvi ye na mo ni baada ya kukataa kuuza mechi kwa zamalek
 
list ya mchongo unamsahau vipi au Meck Maximo katika top 10
 
Kama Pius Nyamko na Hussein Mafta wa Pamba FC hawamo basi list ni feki
 
Wafuatao kwa maoni yangu ndio makocha bora kwa kipindi chote cha uhai wa Tanzania na sio kama alivyotaka mleta nyuzi yaani kuanzia 1990.
  • Victor Stanculescu (Romanian) – Young Africans Coach 1971 to 1974, huyu ndiye kocha bora kwangu kuwahi kufundisha kandanda hapa nchini. Aliipa Yanga ubingwa mara tatu 1971, 1973 na 1974. Alikuza kipaji cha mchezaji bora kuwahi kutokea Tanzania Sunday Manara, lakini kama haitoshi yeye ndiye mwanzilishi wa timu za watoto, aliunda kikosi cha Yanga Kids kwa watoto alio watoa mitaani na kuwafundisha soka na baadaye wakaja kuwa nyota wakubwa sio Tanzania tu hata barani ulaya. Nyota hao ni Juma Pondamali, Jaffar Abdulrahman, Mohammed Mkweche, Mohammed Rishard Adolph, Bona Max, Gordian Mapango, Mohammed Yahya “Tostao”, Kassim Manara na wengine. Kasim Manara na Tostao baadaye walicheza kwa mafanikio nchini Austria, sema wakati huo hatukua na mitandao ya kutupa taarifa kama kipindi cha kina Samata. Victor miaka ya 2000 mwanzoni alikuja tena Tanzania kama kocha wa Taifa stars, awamu hii akiwa mmarekani lakini alikaa miezi miwili tu akaondoka mwenyewe baada ya kuona uswahili mwingi.
  • Paul West Gwivaha (Mtanzania) – Simba SC 1974 na Taifa Stars Coach 1973. Huyu nampa no 2, alikuwa ni kocha wa Taifa Stars, lakini FAT waliipa Simba kocha huyo aifundishe katika kugombea kombe la klabu bingwa 1974. Nakumbuka mwaka 1973 akiwa kocha wa Taifa Stars Tanzania ilifuzu kushiriki michuano ya All Africa Games siyo AFCON iliyofanyika Lagos Nigeria 1973. Baada ya kushiriki mashindano hayo Wachezaji wawili wa Taifa Stars Maulid Dilunga na Omar Mahadhi Bin Jabir walichaguliwa timu ya Africa iliyowakilisha katika michuano ya mabara iliyofanyika Mexico 1973. Akiwa kocha wa Simba 1974, aliiwezesha Simba kufika hatua ya nusu fainali klabu bingwa ya Africa, hatua ambayo haijafikiwa na klabu yoyote hapa nchini. Simba ilikuwa na uwezo wa kuchukua kombe mwaka huo, lakini walifanyiwa vurugu nyingi na klabu ya Mehalla Al kubra ya Misri, ikiwemo kipa wa Simba athumani Mambosasa kuvamiwa na mashabiki na kutishiwa kisu, Simba ilitolewa kwa penalty. Wakati penalty zikipigwa washabiki wa Mehalla walikuwa nyuma ya goli wakimzodoa Mambosasa. Chini ya Gwivaha 1974, Simba walikuwa wakicheza kandanda safi sana, Gwivaha alifanikisha kupandisha viwango vya wachezaji kama Kibadeni, Saad Ally na Mambosasa. K sana atika hatua ya robo fainali Simba iliitoa timu tishio barani Africa wakati huo Accra Hearts of Oak ya Ghana iliyokuwa na washambuliaji hatari sana wakati huo kama Mama Acquah na mohammed Pollo.
Makocha 8 waliobakia ambao kama nitapata muda nitaeleza sifa na mafanikio yao

  • Abdallah Kibadeni
  • Joel Bendera
  • Dragan Popadic
  • Tambwe Leya
  • Nabby Camara
  • James Siang’a
  • Rudy Gutenderndoff
  • Gomez
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…