President wa yanga amecheza mpira wapi?,na soma hii President Magufuli hajawahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi!!!,judge kwa performance not Gender pls
Mdau haujui Engineer Hersi Said amechezea timu za shuleni na chuoni akiwa DIT, kaupiga sana mpira na akina Shaffih Dauda. Hersi amefanya kazi na watu wanaolijua soka kwa muda mrefu kama Senzo na akina Dr.Mshindo tofauti Barbra juu yake kulikuwa na Mo na sasa Try Again wote hawana uzoefu mkubwa kwenye soka kama akina Senzo na Msola.
Hersi hakuanzia nafasi kubwa Yanga alianza kujifunza chini ya wazoefu takribani misimu 2 kisha wa 3 akasogea juu. Ilikuwa seamless integration.
Raisi wa CAF ndugu Patrice Motsepe amejihusisha kwenye soka wa muda mrefu kidogo kiasi cha kumiliki timu ya Mamelodi Sundowns ikafanikiwa sana. Hakuanza kwenye nafasi kubwa ya CAF kutoka kusikojulikana kama Barbra alivyo anza na CEO wa Simba kutoka 'kusikojulikana kisoka'.
Motsepe amenza kufanya kazi za kiungozi na umiliki wa biashara kwa muda mrefu kabla ya kuingia kwenye soka, Barbra hajafikia uzoefu huo wa uongozi.
Yanga wanapata ushauri pia toka kwa wazoefu wa La Liga Spain kuhusu kuendesha kisasa klabu ya mpira hasa ya umiliki wa wanachama.
Yanga haifanyi vizuri kwa sasa kwa kubahatisha kama enzi za Manji kuna mpango mkakati wanao ufuata, kuna clear Visions(Visheni) na malengo (Goals and mile stones) wanafuata. Kuna well written blueprint ambayo kila wanachofanya kimo humo, hata mkakati wa kuandikisha wanachama na mashabiki, uuzaji wa merchandise zao ni bussiness plan iliyo sanifiwa vyema.
Niambie club gani ina run smoothly kuliko Yanga kwenye nyanja hizo nilizosema?
Yanga wanauza jezi na kukusanya ada za uanacha na ushabiki kwa kasi kubwa sana. Wanajiendesha kama corporate kwa sasa. Yanga inaenda kuwa lidubwasha au lidudu likubwa sana ndani ya miaka 10 toka sasa kama hawatavurugana au hawataingia viongozi wababaishaji wenye njaa kali au wanasiasa hawataingilia kati na mikosi yao.