Una hakika haijachakachuliwa ??
Toleo la King James Version lililazimika kushindana na Biblia ya Geneva Bible (1560) juu ya kutumiwa na watu wengi; lakini hatimaye lilienea, na kwa zaidi ya karne mbili na nusu hakuna tafsiri ya Biblia kwa Kingereza iliyoandikwa na kuidhinishwa.
Toleo la King James Version likawa ndilo "toleo lililoidhinishwa" kwa wanaoongea Kingereza…
Ndio, Toleo la King James Version lina dosari kubwa mno.
Kufikia katikati ya karne ya kumi na tisa, maendeleo ya tafiti za Kibiblia vilevile kugunduliwa kwa miswada mingi ambayo ni ya kale zaidi kuliko ile iliyotegemewa na Toleo la King James Version, yamefanya toleo hilo kuwa ni wazi kuwa lina dosari nyingi na mbaya mno na kusababisha kuitishwa kufanyika marekebisho ya tafsiri ya kingereza.
Kazi ikafanywa, kwa idhini ya Kanisa la Uingereza, mwaka 1870
. Toleo la Biblia la English Revised Version lilichapwa mwaka 1881 – 1885; na Toleo la American Standard Version, lahaja zake zimejiingiza katika upendeleo wa wanazuoni wa Kimarekani walioshiriki katika kazi hiyo, nalo lilichapishwa mwaka 1901."
Toleo la King James Version la Agano Jipya liliegemea matini za kigiriki zilizovurugwa kimakosa, ikiwemo kujilimbikizia makosa ya karne ya kumi na nne ya kunukuu miswada.
Nalo kimsingi, lilikuwa ni matini ya Kigiriki ya Agano Jipya kama lilivyoandikwa na Beza, 1589, ambaye kwa ukaribu zaidi alifuata chapa hiyo ya Erasmus, 1516 – 1535, iliyoegemea juu ya miswada ya zama za kati.
Mswada wa kwanza na ulio bora zaidi miongoni mwa miswada minane aliyoishirikisha ulikuwa ni wa karne ya kumi, naye akautumia kidogo mno mswada huo kwa sababu unatofautiana sana na matini za kawaida zilizopokelewa;
Beza alipata miswada miwili ya thamani kubwa mno, ikiwa ni ya karne ya tano na ya sita, lakini aliitumia kidogo go mno kwa sababu inatofautiana na matini iliyochapwa ya Erasmus."
… Toleo la American Standard Version lilipewa haki miliki ya kuzuia matini yake isibadilishwe bila idhini.
Mnamo 1928 haki hiyo ilipatikana kutoka katika Baraza la Kimataifa la Elimu na Dini, na kwa hiyo likawekwa katika umiliki wa makanisa ya Marekani na Canada yaliyoshiriki katika baraza hilo kwa kupitia bodi zao za elimu na uchapaji.
Baraza hilo liliainisha kamati ya wasomi kusimamia matini ya ya Toleo la American Standard Version na kufanya uchunguzi na kujua kama marekebisho zaidi yanahitajika… [Baada ya miaka miwili] uamuzi ulifikiwa; nao ni kuwa; kunahitaji marekebisho kikamilifu katika toleo la 1901, ambalo litabakia kuwa lipo karibu na mapokeo ya Tyndale-King James kama itakavyokuwa… Mnamo 1937 na marekebisho yalipewa idhini kwa kura ya Baraza hilo.