Haya ndo mnafundishwa kule MUM?Sasa mbona mamake na huyu mwanaharam kaandikwa mara nyingi zaidi kwenye kitabu kisicho na shaka ndani yake?Na swali langu bado hujajibu.Huyu Yesu ndo Issa aliyeshusha enjiil?
Sisi Waislamu tunaamini kwamba Bwana Yesu a.s. alikuwa Nabii wa Mungu. Na manabii wote ni watukufu na wapendwa wa Mwenyezi Mungu.
Wanatoka kutoka koo takatifu. Kuhusu ukoo wa Bwana Yesu Kristo Masihi Mwana wa Mariamu a.s. Qur'an Tukufu inaeleza kwamba:
A. Masihi bin Mariamu siye ila ni Mtume tu, bila shaka mitume wote wamekwisha fariki kabla yake, na mama yake ni mwanamke mkweli. (Qur'an 5:76).
B. (Ewe Mariam) baba yako hakuwa mtu m’baya wala mama yako hakuwa asherati. (Qur'an 19:29).
Kwa hiyo sawa na mafundisho ya dini ya Kiislamu tunamheshimu Nabii Isa a.s. (Yesu Kristo) na vile vile wazee wake.
Sisi tunashangaa sana wakati tunaposoma Biblia, tunaona Biblia inamfedhehesha Yesu Kristo vibaya sana.
Licha ya kuwa Mtume wa Mungu sawa na Biblia, Bwana Yesu haonekani hata mtu mwenye ukoo safi, bali tunalazimika kumtafautisha Isa a.s. na Yesu.
Biblia inasema kwamba:
1. Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi mwana wa Ibrahim. (Mathayo 1:1).
2. Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu. (Mathayo 1:5) Rahabu alikuwa kahaba (Yoshua 2:1).
3. Yuda alimzaa Peresi na Zera kwa Tamari (Mathayo 1:3). Tamari alikuwa kahaba na mzinifu. (Mwanzo 38:13-18).
4. Daudi alimzaa Sulemani kwa yule mke wa URIA (Mathayo 1:6). Beth Sheba mkewe URIA alipata mimba ya zinaa. (2 Samuel 11:2-5).
Hawa mabibi wote wa Yesu Kristo walikuwa makahaba na wazinifu.
Lakini sisi hatukubaliani na Biblia bali tunaona kwamba ni taka taka zilizoongezwa katika Biblia.
Na kama Wakristo mnang’ang’ania usahihi wa Biblia, basi mjuwe kwamba Biblia inasema:
“Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana. (Kumb. la Torati 23:2).
Enyi ndugu Wakristo! Kama mnaona kwamba Biblia bado ni sahihi basi mjue kwamba Yesu ni kizazi cha wazinifu, hawezi kuingia katika mkutano wa Mungu.
Kama hawezi hata kuingia katika mkutano wa Mungu, ninyi mnamtegemea nini?
Karibuni, Muhammad s.a.w. mfano wa Musa anawakaribisheni kwa mikono miwili.
Kama mnaona kwamba Yesu Kristo ni mtakatifu lakini Biblia imechafuka kwa mikono ya waandishi, pia karibuni katika dini ya Kiislamu.
Qur'an kitabu cha Mungu kitawatoshelezeni.
Maana hakuna njia ya kusalimika isipokuwa katika dini ya Kiislam. Kwahiyo karibuni sana