Pre GE2025 Makonda ameagizwa na nani kufanya maigizo Nchi nzima!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Paul Makonda anazunguka nchi nzima,anafanya maigizo kwa wananchi, kujidai wanaripoti matatizo kwake na yeye kuyatatua ambapo huenda ,so far amepita sehemu ambazo mteuzi wake hajafika.

Mwenezi anazunguka nchi nzima si KUTATUA kero za wananchi, bali anachokifanya ni kuuonesha umma kuwa hii nchi HAINA Serikali.

Kila anakokwenda raia wamejaa wamemzunguka na shida lukuki! Utakuta eneo lina RC, RAS, DC, DAS, DED mpaka OCD. Bado kuna TAKUKURU, maafisa ardhi, wajumbe wa nyumba 10/10 na kila idara nyeti lakini wote ni USELESS tu.

Wanatafuna tu kodi za wana-nchi! Hata kama ni fedha za CCM -lakini msafara una watu wanaolipwa na serikali ambayo ni fedha za wasio nawa CCM, watendaji wanaacha ofisi wanazurura Makonda kwenye ziara za maigizo kumtangaza mteuzi wake ambaye anajua fika hakubaliki, hakupigiwa kura lakini hata ambaye alipigiwa kura huenda si yeye aliyeshinda.

Kama tuna Mh Majaliwa[waziri mkuu mkali na mchapakazi], haya akaletewa Dotto Biteko [Naibu waziri mkuu] bado inaonekana wana-pwaya na sasa kum'leta Makonda haina shida ,ila sasa kukusanya watu muda wa kazi na kufanya maigizo ni kuwaonea maskini wa kitanzania ambao hawajitambui.

Jamaa anakusanya wananchi wanaoitwa 'wanyonge', halafu anawauliza "haya semeni matatizo yenu mmoja baada ya mwingine!" Kisha wananchi wanawataja viongozi wa maeneo yao kama DC, DED, wenyeviti wa mitaa kama chanzo cha matatizo yao – ambao wote hao ni wana chama tawala!

Cha kushangaza zaidi, Bashite anatoa 'maelekezo' kwa watu HAO HAO waliosababisha matatizo sugu kwa MIAKA yote kwamba waenda WAKAYATATUE ndani ya MASAA au SIKU! Wananchi nao WANAPIGA MAKOFI wakiamini shida zao zimetatuliwa. Utadhani hii ni mara ya kwanza kwa viongozi kufanya haya MAIGIZO! Msafara ukiondoka, kila mtu anarudi nyumbani amechoka, shida ziko pale pale.

Enyi wananchi, muda umefika wa kukataa ujinga kwa vitendo. Muda wa kudai #KatibaMpya
 
wivu tu kwani wewe inakuuma nini
 

Wanaofanyaga maigizo ni kina Lisu, Mbowe, Lema ambao hata ukiwalilia shida gani hawawezi kukisaidia hata kwa elfu 10.
 
Wanaofanyaga maigizo ni kina Lisu, Mbowe, Lema ambao hata ukiwalilia shida gani hawawezi kukisaidia hata kwa elfu 10.
Unaonyesha uchi wako wa akili hapa.
Unamlilia shida mtu ambaye hujamlipa kodi?
Unatoka familia maskini alafu una-roho ya kuombaomba uliyoridhi kwenye serikali kukopa chakula wakati tuna mashamba , mbolea, mabonde na mvua ;maji yanaishia baharini.
 
Swali ni je, Wananchi wanampokeaje? Je Maeneo mengine yanataman pia afike au?.

Kati yako wewe Mmoja na wananchi maelfu Kwa maelfu wanaojitokeza, Ni nani tumzingatie nani tumpuuze?.
 

Kwanini Rais asifanye na kusimamia haki, ukweli na kusimama na kusimamia nchi.

Hivi unafikiri vitu anavyofanya Makonda angefanya rais, umeme ungekatika, maji yangekuwa shida, mfumuko wa bei, za daladala zingepanda kihivyo. Rushwa ingekithiri na unanijua mimi ni nani?

Ni hivi hata wewe ukiwa mkweli, ukitatua shidq za wananchi utapendwa tena sana tu.
 
Wqtanzania zaidi ya 90% ni wajinga na hawa ndiyo mtaji wa CCM.
 
Makonda ni mtendaji kwenye hii nchi?

Samia si anasaidiwa na
1. Mpango [makamu wa Raisi]
2. Waziri mkuu
3. Naibu Waziri Mkuu.
4 . Mawaziri.
5. Makatibu Wakuu.
6. RC<DAS na DC?

Unataka kuuambia Umma wa Tanzania kwamba hawa wote hamna kitu wanafanya hivyo sasa Rasi kaamua kumteua mtu /mwenenzi wa chama[CCM] akawe mtendaji wa serikali?
Mandate ya kuitisha mawaziri na RPC hadharani na kutaka watoe majibu inatoka sheria gani?
#Lawless Country.
Tusubiri siku atamuita jaji mkuu jukwani ajibu kwanini hukumu imema ushindi huyu na kumuacha yule.
 
Wqtanzania zaidi ya 90% ni wajinga na hawa ndiyo mtaji wa CCM.
Na wanaendelea kuzalisha wajinga wengi . Matokeo ya form four hapo Temeke Secondary divishion four na zero ni karibu wanafunzi 400 kwenye shule moja, hao wana ajira ya moja kwa moja kubeti na bodaboda na ndio mtaji wa CCM.
 

Umeshaangalia Magufuli na Makonda wanasikiliza nini? Na wanatatua nini?

Ni hivi alisimia kubwa ya watanzania maskini, wajane, yatima wananchi wanaporwa ardhi, kitu chochote cha thamani walichonacho. Hao ni 80% ya Watanzania.

Ukitaka kuwa maarufu hata leo simamia haki, tembea wasikilize wananchi. Ondoa viongozi mafia kwenye maeneo yao.
 
hiki anachokifanya Makonda kilitakiwa kufanywa na wanasiasa wa upinzani kama chadema na wengine hakika wangepata wabunge wengi na hata nchi wangeitawala ila kinachotokea ni ccm kuendelea kutawala wenyewe maan wanang'ata na kupuliza na wananchi wala hawashtuki...!
 
Hivi Makonda analindwa na TISS? Naona kuna jamaa wanamlinda kwa ukaribu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…