Paul Makonda anazunguka nchi nzima,anafanya maigizo kwa wananchi, kujidai wanaripoti matatizo kwake na yeye kuyatatua ambapo huenda ,so far amepita sehemu ambazo mteuzi wake hajafika.
Mwenezi anazunguka nchi nzima si KUTATUA kero za wananchi, bali anachokifanya ni kuuonesha umma kuwa hii nchi HAINA Serikali.
Kila anakokwenda raia wamejaa wamemzunguka na shida lukuki! Utakuta eneo lina RC, RAS, DC, DAS, DED mpaka OCD. Bado kuna TAKUKURU, maafisa ardhi, wajumbe wa nyumba 10/10 na kila idara nyeti lakini wote ni USELESS tu.
Wanatafuna tu kodi za wananchi! Hata kama ni fedha za CCM -lakinn msafara una watu wanaolipwa na serikali ambayo ni fehda za wasio na wa CCM, watendaji wanaacha ofisi wanazurura naye kwenye ziara ya maigizo kumtangaza mteuzi wake.
Kama tuna Mh Majaliwa[waziri mkuu mkali na mchapakazi], haya akaletewa Dotto biteko[Naibu waziri mkuu] bado inaonekana wanapwaya na sasa kumleta Makonda haina shida ila sasa kukusanya watu muda wa kazi na kufanya maigizo ni kuwaonea maskini wa kitanzani.
Jamaa anakusanya wananchi wanaoitwa 'wanyonge', halafu anawauliza "haya semeni matatizo yenu mmoja baada ya mwingine!" Kisha wananchi wanawataja viongozi wa maeneo yao kama DC, DED, wenyeviti wa mitaa kama chanzo cha matatizo yao – ambao wote hao ni wana chama tawala!
Cha kushangaza zaidi, Bashite anatoa 'maelekezo' kwa watu HAO HAO waliosababisha matatizo sugu kwa MIAKA yote kwamba waenda WAKAYATATUE ndani ya MASAA au SIKU! Wananchi nao WANAPIGA MAKOFI wakiamini shida zao zimetatuliwa. Utadhani hii ni mara ya kwanza kwa viongozi kufanya haya MAIGIZO! Msafara ukiondoka, kila mtu anarudi nyumbani amechoka, shida ziko pale pale.
Enyi wananchi, muda umefika wa kukataa ujinga kwa vitendo. Muda wa kudai #KatibaMpya