Makonda amuomba Mabeyo amuwakilishe siku ya kumbukizi ya Hayati Magufuli

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, amemtembelea Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kutumia nafasi hiyo kumshukuru kwa mchango wake mkubwa kwa taifa pamoja na kulea viongozi wengi wanaolitumikia taifa katika nyanja mbalimbali. Makonda amesema Watanzania wanaendelea kujivunia kazi na uzalendo aliouonesha Jenerali Mabeyo wakati wa utumishi wake, huku akiendelea kumuombea afya njema ili aweze kufurahia matunda ya jasho lake.

Katika mazungumzo yao, Makonda pia alizungumzia kumbukizi ya miaka mitano tangu kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, zitakazofanyika Chato mkoani Geita. Waziri Makonda alimuomba Jenerali Mabeyo kuhudhuria kumbukizi hizo na kufikisha salamu zake, akisisitiza kuwa uzalendo, uadilifu na mapenzi ya Hayati Magufuli kwa Watanzania bado yanaendelea kuishi mioyoni mwa wengi.

Makonda amesema licha ya changamoto mbalimbali zinazoibuka katika jamii, taifa linaendelea kubaki imara na lenye mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza maadili ya utumishi, uwajibikaji na kuwatetea wanyonge kama alivyofanya Hayati Magufuli wakati wa uongozi wake.

Mwandishi, kichwa cha habari kipo sawa?
 
Mabeyo na aliokuwa nao karibu akiwaongoza ni failure wakubwa kupata kutokea duniani kwa kushindwa kuchukua maamuzi magumu na ya faida kwa vizazi vyetu baada ya matukio ya ajabu ajabu yaliyotokea kabla na baada ya 17 March 2021

Yaani haielezeki kwa nafasi yake yeye kushindwa kuwajibika hata sasa tumebaki na balaa kama siyo laana.
 
Ni kweli alizingua ila pia ingeweka precedence mbaya sana, kila Rais angekua anatolewa kwa mapinduzi tu!
 
Hao akina Makonda ni wale marafiki maslahi, kama hakuna anachoweza kufaidika na ww anajifanya yuko busy, wala simu yako hapokei. Magufuli amgekuwa hai na urais wake, shughuli yoyote ya nyumbani kwake Makonda angafika hapo wiki nzima kabla.
 
Alishawekwa pembeni, pona yake ni hicho kifo, waliopo wamemkumbuka.
 
Halafu eti awe waziri mkuu na wengine hata kuthubutu na kudai eti awe ikulu!
WADANDANYIKA tuna mambo ya ajabu sana sana!
Huyu aliyefoji vyeti na mwenye IQ 30 atuongoze kweli?!
 
Back
Top Bottom