Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Madai yote hayo ya kijinai hayajawahi kuthibitishwa.Dogo anapiga kazi ila Ana makando kando mengi sana kuhusu kudhulumu watu kwa mabavu! Kuvunja haki za binadamu! Na pili kutofuata sheria
Britanicca
Mwenye kinga ya kesi ni Rais wa nchi tu, raia mwingine hakwepi viunga vya mahakama.
Na ndiyo sababu tulio mbali na maeneo anayodaiwa kufanyia tuhuma za kijinai huona kuwa hizo ni fitina zenye mrengo wa kumharibia ama kuidhibiti 'pace' yake ya harakati.
Ingawa naelewa kuwa mahakama si vijiwe vya kupigia soga, lakini sasa hata kina Gsm wenye 'ukwasi zao', walifurukuta kidogo tu kisha wakajiondoa wenyewe kushitaki, tena jamaa akiwa keshatoka kabisa madarakani, why why why?
Nishaona Tz kiongozi yeyote mwenye msimamo huzushiwa zengwe lenye tuhuma za kutisha na kuhuzunisha.