Makonda anataka kuitumia Simba kupanda kisiasa zaidi au Mo ndio anamtumia kufikia malengo yake kibiashara?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Mchanganyiko wa mpira na siasa za utawala wa CCM Tanzania ni mojawapo ya jambo la kuudhi sana linalokwamisha na kuharibu mema ya nchi yetu pande zote mbili pamoja na kuleta migawanyiko ambayo hakipaswa kuwepo.

Kuna video clip nimieona ya mwanamke mmoja huenda ni shabiki au kiongozi wa Simba(jina simjui) mnene amevaa ushungi na miwani mikubwa anaongea kwa kuchanganya sana Kingereza na Kiswahili akimshukuru na kumuombea Makonda kirefu sana kwamba amekuja wakati sahihi kutenda haki na zaidi akimuombea siku moja kuwa kiongozi mkubwa zaidi ya hapo katika nchi ili kuleta haki kwa nchi nzima!

Ukimsikiliza huyo mwanamke mambo mengi anayoongea sijui ya Transformation ya Simba na mifano huko nje kwanza ni ulaghai mtupu. Anawadanganya wanasimba wenzake kwamba transformation yao ya Mo kuchukua timu itakuwa kama Manchester City, Chelsea na PSG, nilicheka sana na kusikitika niliposikia huu upupu wake.

Wakati anamalizia porojo zake ndipo akaanza kumwaga sifa, mapambio na shukrani zote kwa Makonda! Hili lilinishangaza zaidi hasa nilipokumbuka kutekwa na kurejeshwa kwa Mo enzi akiwa mkuu wa mkoa.
 
michezo ni afya ndugu hivyo sishangai siasa ikiingia kwani siasa ni maisha na maisha afya ni chanda na pete
 
Ahh hakuna jambo linatokea kwa bahati mbaya hasa haya yanayohusu hizi timu zetu kubwa za Dar.

Kila kitu kinatokea kwa sababu maalumu either za kisasa, kiuchumi ama kujinufaisha kwa namna mbalimbali.

Hapo ndipo unapowaona machawa wanatokea kideoni na redioni kama wasemaji wa timu.

Wanalipwa vipesa vya maji kutimiza malengo makubwa zaidi ya watawala na viongozi wa timu hizo. Aibu!
 
Mchanganyiko wa mpira na siasa za utawala wa CCM Tanzania ni mojawapo ya jambo la kuudhi sana linalokwamisha na kuharibu mema ya nchi yetu pande zote mbili pamoja na kuleta migawanyiko ambayo hakipaswa kuwepo.

Kuna video clip nimieona ya mwanamke mmoja huenda ni shabiki au kiongozi wa Simba(jina simjui) mnene amevaa ushungi na miwani mikubwa anaongea kwa kuchanganya sana Kingereza na Kiswahili akimshukuru na kumuombea Makonda kirefu sana kwamba amekuja wakati sahihi kutenda haki na zaidi akimuombea siku moja kuwa kiongozi mkubwa zaidi ya hapo katika nchi ili kuleta haki kwa nchi nzima!

Ukimsikiliza huyo mwanamke mambo mengi anayoongea sijui ya Transformation ya Simba na mifano huko nje kwanza ni ulaghai mtupu. Anawadanganya wanasimba wenzake kwamba transformation yao ya Mo kuchukua timu itakuwa kama Manchester City, Chelsea na PSG, nilicheka sana na kusikitika niliposikia huu upupu wake.

Wakati anamalizia porojo zake ndipo akaanza kumwaga sifa, mapambio na shukrani zote kwa Makonda! Hili lilinishangaza zaidi hasa nilipokumbuka kutekwa na kurejeshwa kwa Mo enzi akiwa mkuu wa mkoa.
Tulishaachana na mamipira ya bongo
 
Back
Top Bottom