GE2025 Makonda: Anayekushawishi uvunje amani, mwambie akupe kwanza hela ya kula ya miaka 10 ijayo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewaambia wananchi kwamba yeyote anayewashawishi kuandamana badala ya kupiga kura Oktoba 29, 2025, awalipe kwanza fedha za kujikimu kwa kipindi cha miaka 10.

Akizungumza Jumatatu Oktoba 20, 2025, alipokuwa na wafanyabiashara katika Soko la Nyama Choma Kumbilamoto, Kata ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Makonda alisema:

“Mtu akikushawishi uvunje amani mwambie kwanza nipe hela ya kula miaka 10 ijayo. Kama ulikuwa na ndoto kupitia biashara yako ya kuuza mbuzi ujenge nyumba, ununue gari, uwe na mke au mume muishi maisha mazuri, basi mwambie tupigiane hesabu. Nipe changu niweke mfukoni ili likitokea la kutokea, nina uhakika wa maisha yangu miaka 10 ijayo,”
 
Hii amani wanayosema ni amani ya kina Makonda kutumia ufisadi kujitajirisha. Kla siku wanadanganya amani wakati mtaani watu wanaishi maisha magumu huku wenyewe wakijilundikia magari ya bei ghali.

HII NDIYO AMANI YA KINA MAKONDA WANALILIA MSIIVURUGE

1760971887049.jpeg
 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, ameendelea na ziara zake za kampeni kwa ajili ya kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Leo, Oktoba 20, 2025, Makonda amefika katika jiji la Dar es Salaam ambako amekutana na mafundi ujenzi na kufanya mazungumzo nao. Katika mkutano huo, aliwahimiza kujitokeza kwa wingi kumpokea Dkt. Samia Suluhu ambaye anatarajiwa kuwasili jijini humo kesho kwa ajili ya kuendelea na kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza na mafundi hao waliojitokeza kwa wingi, Makonda alieleza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, akisisitiza kuwa ni haki ya kikatiba ambayo hufanyika kila baada ya miaka mitano. Alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na kufuata misingi ya katiba bila kuruhusu mtu yeyote kuvuruga mchakato huo. Pia Makonda alieleza mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu katika Serikali ya Awamu ya Sita, akibainisha kuwa hatua hizo ni ushahidi tosha wa uongozi imara unaojali wananchi, hivyo ni muhimu kumpa tena ridhaa ya kuongoza kwa awamu nyingine. Aidha aliwahimiza mafundi ujenzi pamoja na wananchi wote kwa ujumla kutumia haki yao ya kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaoendana na matakwa yao na kuendeleza maendeleo ya taifa.
Na nyie mnaoambiwa mdai pesa ya kula miaka 10,mngemtaka kwanza awaambie yeye tayari anayo hela ya kula miaka mia ngapi au elfu ngapi?Kwani maisha haya ukikibali kuburuzwa jua wewe hata kuingia peponi haustahili!
 
Tunaowalipa Kodi na hawafanyi wanachotakiwa kufanya hivyo wengi mtaani kuwa mafukara ndio wanataka kuvunja Amani - Wanakula jasho letu with nothing to show for it - Hii inanikumbusha msemo wa Nyani haoni Kundule
 
Aaah mtawavurugia amani ya kula bata na mapesa yao au sio???
 
Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewaambia wananchi kwamba yeyote anayewashawishi kuandamana badala ya kupiga kura Oktoba 29, 2025, awalipe kwanza fedha za kujikimu kwa kipindi cha miaka 10.

Akizungumza Jumatatu Oktoba 20, 2025, alipokuwa na wafanyabiashara katika Soko la Nyama Choma Kumbilamoto, Kata ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Makonda alisema:

“Mtu akikushawishi uvunje amani mwambie kwanza nipe hela ya kula miaka 10 ijayo. Kama ulikuwa na ndoto kupitia biashara yako ya kuuza mbuzi ujenge nyumba, ununue gari, uwe na mke au mume muishi maisha mazuri, basi mwambie tupigiane hesabu. Nipe changu niweke mfukoni ili likitokea la kutokea, nina uhakika wa maisha yangu miaka 10 ijayo,”

Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewaambia wananchi kwamba yeyote anayewashawishi kuandamana badala ya kupiga kura Oktoba 29, 2025, awalipe kwanza fedha za kujikimu kwa kipindi cha miaka 10.

Akizungumza Jumatatu Oktoba 20, 2025, alipokuwa na wafanyabiashara katika Soko la Nyama Choma Kumbilamoto, Kata ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Makonda alisema:

“Mtu akikushawishi uvunje amani mwambie kwanza nipe hela ya kula miaka 10 ijayo. Kama ulikuwa na ndoto kupitia biashara yako ya kuuza mbuzi ujenge nyumba, ununue gari, uwe na mke au mume muishi maisha mazuri, basi mwambie tupigiane hesabu. Nipe changu niweke mfukoni ili likitokea la kutokea, nina uhakika wa maisha yangu miaka 10 ijayo,”
Huyu chawa atakuja kufa kifo kibaya kama waliomtengeneza yaani Samuel Sitta na John Magufuli.
 
Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewaambia wananchi kwamba yeyote anayewashawishi kuandamana badala ya kupiga kura Oktoba 29, 2025, awalipe kwanza fedha za kujikimu kwa kipindi cha miaka 10.

Akizungumza Jumatatu Oktoba 20, 2025, alipokuwa na wafanyabiashara katika Soko la Nyama Choma Kumbilamoto, Kata ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Makonda alisema:

“Mtu akikushawishi uvunje amani mwambie kwanza nipe hela ya kula miaka 10 ijayo. Kama ulikuwa na ndoto kupitia biashara yako ya kuuza mbuzi ujenge nyumba, ununue gari, uwe na mke au mume muishi maisha mazuri, basi mwambie tupigiane hesabu. Nipe changu niweke mfukoni ili likitokea la kutokea, nina uhakika wa maisha yangu miaka 10 ijayo,”
 
..hata kupiga kura kama mtu hulipwi donge nono ni utakuwa mpumbavu.
 
Back
Top Bottom