Makonda aomba kupangiwa kazi nyingine Januari 2025

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuanzia sasa hadi Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi ya kuwanyoosha watumishi wa umma wasiokuwa wazalendo na wanaotanguliza masilahi yao binafsi.

Makonda amemwomba Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenda kumwombea kwa Rais Samia Suluhu Hassan amvumilie kwa kipindi hiki cha miezi sita.

Amesema hayo leo Jumatatu, Juni 3, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Dk Nchimbi uliofanyika Soko la Kilombero, Arusha Mjini.

"Nikuhakikishie katibu mkuu, watakula spana za kutosha,”amesema Makonda.
Pia, amesema na ikifika Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi na kama kutakuwa na mkoa mwingine yuko tayari kupelekwa.

Makonda amesema:"Amekuta mkoa huo kuna watumishi wasiokuwa wazalendo, hawataki kujituma, sio wote ila wengi wao wanatumia masilahi yao binafsi, naomba kaniombee kwa Rais, anivumilie kidogo, mfunge masikio nipige spana ili haki za wananchi zipatikane."

Katika kusisitiza hilo, Makonda amesema:"Nitawanyoosha mpaka kieleweke na ikifika Januari 1, 2025 utakuwa mkoa wa mfano."

Amesema kuna zaidi ya Sh20 bilioni zinazoweza kurudi serikalini zilizotolewa ili kutekeleza miradi mbalimbali lakini hazijatumika pasi na sababu za msingi huku wananchi wakilia kukosa huduma za afya, maji na elimu na hayuko tayari kuona hilo likitokea.
 
kama ni kweli, mkoa umepangiwa Bi 21 wakatumia Bi moja na Bi 20 wanarudisha, halafu mwaka ujao wa fedha wapangiwe tena Bi 21, inamaana watakuwa wamepewa Bi 1 (na kurudishiwa zile 20 walizorudisha)???
Huku kuna miradi kibao ya Hospitali na mashule yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi kwa kukosa fedha???
Kuna shida sana huku mikoani...zinazohitaji kutengenezewa dawa/suluhisho la kudumu...
 
Wataalamu wa kufungua Code tumemuelewa Makonda anamaanisha kwamba Rais amfikirie 2025-2030 ampe nafasi ya Uwaziri Mkuu

Sent from my SM-G998U using JamiiForums mobile app
Akikomaa kidogo kiakili hiyo nafasi ya Waziri mkuu inamfaa. Waziri mkuu hapaswi kupoa kama uji wa mchele, waziri mkuu anapaswa kuwa moto wa kuotea mbali. Kama akina Sokoine, na kwa wale ambao ni kizazi cha 2000s watamtolea mfano Lowassa.

Waziri mkuu anatakiwa kuwa kama hivyo vyuma viwili hapo juu, na sijui ilipangwa, wote wametokea jimbo moja na wameongoza chini ya JK's.

Nimesema uwaziri mkuu kwakuwa kutakuwa na mtu juu yake wa kumtuliza pale kichwa kitakapowaka moto. Ni kama Magufuli, angefaa zaidi katika nafasi ya PM.
 
Nimesema uwaziri mkuu kwakuwa kutakuwa na mtu juu yake wa kumtulia pale kichwa kitakapowaka moto. Ni kama Magufuli, angefaa zaidi katika nafasi ya PM.
Sahihi kabisa

Sent from my SM-G998U using JamiiForums mobile app
 
Akikomaa kidogo kiakili hiyo nafasi ya Waziri mkuu inamfaa. Waziri mkuu hapaswi kupoa kama uji wa mchele, waziri mkuu anapaswa kuwa moto wa kuotea mbali. Kama akina Sokoine, na kwa wale ambao ni kizazi cha 2000s watamtolea mfano Lowassa.

Waziri mkuu anatakiwa kuwa kama hivyo vyuma viwili hapo juu, na sijui ilipangwa, wote wametokea jimbo moja na wameongoza chini ya JK's.

Nimesema uwaziri mkuu kwakuwa kutakuwa na mtu juu yake wa kumtuliza pale kichwa kitakapowaka moto. Ni kama Magufuli, angefaa zaidi katika nafasi ya PM.
Ila sharti awe PM na afanye kazi ya U pm ila akirigwa kutumia nafasi ya PM kusaka Urais ataliwa kichwa kama hoa hoa uliowataja
 
Urais ni taasisi yenye wivu sana, wapambe wa anayeongoza hiyo taasisi nao wanachangia pia.

Mtu anaweza akawa anatimiza vyema majukumu yake kama waziri mkuu, hasa ukizingatia ukubwa wa madaraka ya waziri mkuu, basi Rais akaanza kuona kama anafunikwa au Urais wake upo shakani.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuanzia sasa hadi Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi ya kuwanyoosha watumishi wa umma wasiokuwa wazalendo na wanaotanguliza masilahi yao binafsi.

Makonda amemwomba Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenda kumwombea kwa Rais Samia Suluhu Hassan amvumilie kwa kipindi hiki cha miezi sita.

Amesema hayo leo Jumatatu, Juni 3, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Dk Nchimbi uliofanyika Soko la Kilombero, Arusha Mjini.

"Nikuhakikishie katibu mkuu, watakula spana za kutosha,”amesema Makonda.
Pia, amesema na ikifika Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi na kama kutakuwa na mkoa mwingine yuko tayari kupelekwa.

Makonda amesema:"Amekuta mkoa huo kuna watumishi wasiokuwa wazalendo, hawataki kujituma, sio wote ila wengi wao wanatumia masilahi yao binafsi, naomba kaniombee kwa Rais, anivumilie kidogo, mfunge masikio nipige spana ili haki za wananchi zipatikane."

Katika kusisitiza hilo, Makonda amesema:"Nitawanyoosha mpaka kieleweke na ikifika Januari 1, 2025 utakuwa mkoa wa mfano."

Amesema kuna zaidi ya Sh20 bilioni zinazoweza kurudi serikalini zilizotolewa ili kutekeleza miradi mbalimbali lakini hazijatumika pasi na sababu za msingi huku wananchi wakilia kukosa huduma za afya, maji na elimu na hayuko tayari kuona hilo likitokea.
Comedy show inaendelea kama Kawa
 
kama ni kweli, mkoa umepangiwa Bi 21 wakatumia Bi moja na Bi 20 wanarudisha, halafu mwaka ujao wa fedha wapangiwe tena Bi 21, inamaana watakuwa wamepewa Bi 1 (na kurudishiwa zile 20 walizorudisha)???
Kumbe!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuanzia sasa hadi Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi ya kuwanyoosha watumishi wa umma wasiokuwa wazalendo na wanaotanguliza masilahi yao binafsi.

Makonda amemwomba Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenda kumwombea kwa Rais Samia Suluhu Hassan amvumilie kwa kipindi hiki cha miezi sita.

Amesema hayo leo Jumatatu, Juni 3, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Dk Nchimbi uliofanyika Soko la Kilombero, Arusha Mjini.

"Nikuhakikishie katibu mkuu, watakula spana za kutosha,”amesema Makonda.
Pia, amesema na ikifika Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi na kama kutakuwa na mkoa mwingine yuko tayari kupelekwa.

Makonda amesema:"Amekuta mkoa huo kuna watumishi wasiokuwa wazalendo, hawataki kujituma, sio wote ila wengi wao wanatumia masilahi yao binafsi, naomba kaniombee kwa Rais, anivumilie kidogo, mfunge masikio nipige spana ili haki za wananchi zipatikane."

Katika kusisitiza hilo, Makonda amesema:"Nitawanyoosha mpaka kieleweke na ikifika Januari 1, 2025 utakuwa mkoa wa mfano."

Amesema kuna zaidi ya Sh20 bilioni zinazoweza kurudi serikalini zilizotolewa ili kutekeleza miradi mbalimbali lakini hazijatumika pasi na sababu za msingi huku wananchi wakilia kukosa huduma za afya, maji na elimu na hayuko tayari kuona hilo likitokea.
Nenda Mwanza bashite ukawanyooshe akina mangosha
 
Back
Top Bottom