Makonda aomba kupangiwa kazi nyingine Januari 2025

Makonda aomba kupangiwa kazi nyingine Januari 2025

Mshahara wa RC ni million 4, toa matumizi Kwa mwezi assume anatumia Milioni 2.5,

Ametoa wapi pesa ya kujenga ghorofa kama Si wizi!!

Endelea kudanganywa!!
Kwani RC hana posho za safari na zingine nyingi? Kama mtu wa kawaida tena CHAWA tu kama Mwijaku anajenga ghorofa sembuse RC?
 
Naona anaanza kutamani ile kazi ya enzi ya kupoteza raia na waandishi wa habari.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuanzia sasa hadi Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi ya kuwanyoosha watumishi wa umma wasiokuwa wazalendo na wanaotanguliza masilahi yao binafsi.

Makonda amemwomba Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenda kumwombea kwa Rais Samia Suluhu Hassan amvumilie kwa kipindi hiki cha miezi sita.

Amesema hayo leo Jumatatu, Juni 3, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Dk Nchimbi uliofanyika Soko la Kilombero, Arusha Mjini.

"Nikuhakikishie katibu mkuu, watakula spana za kutosha,”amesema Makonda.
Pia, amesema na ikifika Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi na kama kutakuwa na mkoa mwingine yuko tayari kupelekwa.

Makonda amesema:"Amekuta mkoa huo kuna watumishi wasiokuwa wazalendo, hawataki kujituma, sio wote ila wengi wao wanatumia masilahi yao binafsi, naomba kaniombee kwa Rais, anivumilie kidogo, mfunge masikio nipige spana ili haki za wananchi zipatikane."

Katika kusisitiza hilo, Makonda amesema:"Nitawanyoosha mpaka kieleweke na ikifika Januari 1, 2025 utakuwa mkoa wa mfano."

Amesema kuna zaidi ya Sh20 bilioni zinazoweza kurudi serikalini zilizotolewa ili kutekeleza miradi mbalimbali lakini hazijatumika pasi na sababu za msingi huku wananchi wakilia kukosa huduma za afya, maji na elimu na hayuko tayari kuona hilo likitokea.
wakuu sijaelewa kabisa yaan Mkoa unatengewa b zaidi ya 20 halaf wenyew unatumia moja tuu kwa mwaka wa fedha ama!?
Aisee pamoja na changamoto zoote hizi daah tunasafar ndefu sana.Na hapo ni Arusha tu je kwenye hii mikoa mingine hali ipoje?Najiuliza hv Majaliwa kazi yake kubwa ni KUPAKA PIKO tu ama n nini?Hii aibu sana yaan
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuanzia sasa hadi Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi ya kuwanyoosha watumishi wa umma wasiokuwa wazalendo na wanaotanguliza masilahi yao binafsi.

Makonda amemwomba Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenda kumwombea kwa Rais Samia Suluhu Hassan amvumilie kwa kipindi hiki cha miezi sita.

Amesema hayo leo Jumatatu, Juni 3, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Dk Nchimbi uliofanyika Soko la Kilombero, Arusha Mjini.

"Nikuhakikishie katibu mkuu, watakula spana za kutosha,”amesema Makonda.
Pia, amesema na ikifika Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi na kama kutakuwa na mkoa mwingine yuko tayari kupelekwa.

Makonda amesema:"Amekuta mkoa huo kuna watumishi wasiokuwa wazalendo, hawataki kujituma, sio wote ila wengi wao wanatumia masilahi yao binafsi, naomba kaniombee kwa Rais, anivumilie kidogo, mfunge masikio nipige spana ili haki za wananchi zipatikane."

Katika kusisitiza hilo, Makonda amesema:"Nitawanyoosha mpaka kieleweke na ikifika Januari 1, 2025 utakuwa mkoa wa mfano."

Amesema kuna zaidi ya Sh20 bilioni zinazoweza kurudi serikalini zilizotolewa ili kutekeleza miradi mbalimbali lakini hazijatumika pasi na sababu za msingi huku wananchi wakilia kukosa huduma za afya, maji na elimu na hayuko tayari kuona hilo likitokea.

ubunge huo
 
Makonda ananamna fulani ya uongozi ambao hakuna mahali atakaa asitoshe... na hili wanalo sana watu wenye mchanganyiko wa haiba ya sanguine na colerick hawa watu huwa wanazalisha tabia ya uthubutu wa ajabu mnoo! Wapo wachache sana duniani na Bahati mbaya sana huwa wakati mwingine hawadumu sana!

sasa bila kuathiri makusudi ya ajenda makonda anazo hizo haiba kinacho niogopesha tu ni kwamba anajitengenezea maadui wachache ambao wananguvu kifedha na kimamlaka na pale ambapo akiingia katika 18 zao inaweza kumuwia ngumu kutambaa kwenye tope zito bila kuzama!

Rai yangu kwa makonda atende kwa kadri ambavyo haki itapatikana kwa kila mmoja ila asisahau katika kutenda haki kwake kunawatu hawafurahishwi...

Natamani kumwambia jambo ila kwa sasa tukubali kuwa Arusha ndyo wananufaika zaidi na makonda kuliko makonda atakavyo nufaika na Arusha, mengine tumwaachie Mungu wetu

Mr bon
 
Umechelewa sana huyu ni kiongozi ambaye anajua mpaka anapitiliza
 
Shida ni mfumo wa ajira jwabwatumishi
 
kama ni kweli, mkoa umepangiwa Bi 21 wakatumia Bi moja na Bi 20 wanarudisha, halafu mwaka ujao wa fedha wapangiwe tena Bi 21, inamaana watakuwa wamepewa Bi 1 (na kurudishiwa zile 20 walizorudisha)???
Huku kuna miradi kibao ya Hospitali na mashule yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi kwa kukosa fedha???
Kuna shida sana huku mikoani...zinazohitaji kutengenezewa dawa/suluhisho la kudumu...
Hizi ishu za kurudisha pesa wanapenda sana watumishi sijui ni kwanini aisee.
 
Nashauri apewe uwaziri wa Tamisemi, maana madudu mengi au yote yapo Tamisemi kwa miaka mingi sana sasa.
 
Back
Top Bottom