Uchaguzi 2020 Makonda apiga kambi ubunge Kigamboni

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Licha ya Polepole kuwaonya wateuliwa wanaowinda ubunge wa Kigamboni taarifa za ndani zinasema bado Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mheshimiwa Makonda anapitapita kutafuta ubunge Kigamboni.

Kwa sasa mbunge wa kigamboni ni Faustine Ndugulile wa CCM.

Tazama pia kauli ya Polepole aliyoitoa miezi michache iliyopita

 
Naona bavicha mko bize kuwasemelea wale vijana wa sisiemu ambao wanawalaza na viatu. Kuna mwenzako katoka kumsemelea gambo na kina mnyeti wa arusha muda si mrefu na bado, hawa vijana ni wanakula nanyi sahani moja, hamna namna, hamna namna mnaenda wakwepa!, na ali hapi bado hajaanza kuwashindilia.
 
Alianza kupitapita jimbo la Kawe, kamwaga vihela vyake uchwara but kakuta wakazi wa jimbo hilo wanajitambua wakabaki wanamwangalia kama hawamuoni vile - zero shobo yaani.

naona sasa kaenda kapeleka litmus test jimbo la Kigamboni.
 
Kwa wakazi wa Kigamboni nakiri kusema itakuwa furaha sana kama Mh Makonda akiwa mbunge kupitia jimbo hili, maana huyu jamaa yupo karibu sana na Mh Raisi hvyo atatumia ukaribu huo kufanya ushawishi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii ktk jimbo hili..!!!

Win Win situation, tumpe ubunge tukimbie kimaendeleo

Licha ya mapungufu yake lakn Baniani mbaya kiatu chake dawa
 
Hivi mbunge wa jimbo na mkuu wa huo mkoa nani mkubwa au target ni uwaziri? Na je waziri na mkuu wa mkoa nani mkubwa? Au Target ni uspika?
Mkuu wa Mkoa Hana uhakika na ajira yake kama ilivyo kwa Gambo leo inategemea na maamuzi ya aliekuteua.

Mbunge uhakika Mishahara Mkubwa, marupurupu na posho kubwa kubwa mwisho wa siku baada ya miaka mitano inapewa zaidi ya milioni 200 kiinua mgongo.

Isitoshe mbunge sio Mtendaji yeye kupiga mdomo tu kama Mlinga Msukuma ama Lusinde halafu unaonekana shujaa..
 
Unamjua tayari Rais wa 2020-25?
 
Ukiwa mbunge ni kifo tu ndio kitakuondoa au ufukuzwe uanachama.
Ila ukuu wa mkoa siku JPM akiamka vibaya hauna chako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…