Makonda asimulia Jenerali Mabeyo alivyomuokoa kwenye sakata la makontena

Ama hakika Mungu ana kazi sana, kumbe kuna maombi ya kusambaratisha vikao vya usiku?

Hivi hio vita aliyo kuwa anapogwa ni kutoka jwa watu nje ya ccm ama ndani?

Ajabu mpiga vita nae alipigwa vita!

Iko wazi ni kutoka ndani ya ccm
 
kukaaa kimyaa nalo n jibu
Mh wangu makondaa jitahidi kusahau ya nyumaa mengine yanaweza kuharibu future Mungu aliokuwekea mbelen

ushauritu
Nkumbushe ulisema ulivyochaguliwa pale lumumba nimewasamehee wotee na kuwasahauuuuuuuuuuuuuuu

Mungu aliandoka hili neno kwenye kitabu chake akiamini ulichosema tusamehe maadui zetuu tuweze kutoboa zaidi
 
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesimulia namna alivyookolewa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo katika sakata la makontena ya vifaa vya ofisi za walimu wa Dar es Salaam kwa kuwa kuna watu walitaka kumchomekea matrekta na magari kwenye makontena hayo.

Makonda aliyasema hayo jana jijini hapa alipokutana na wadau wa mashirika na asasi za kiraia kujadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo changamoto zinazowakabili.

Alisema pona yake ni Jenerali Mabeyo kuzuia makontena yasifunguliwe na ulinzi kuendelea kuimarika, la sivyo matrekta na magari yangewekwa katika makontena hayo ili ionekane hakuleta thamani bali ni magari yake.

“Kipindi kile namshukuru Mungu baada ya kugundua taarifa walizozipeleka kwa Rais John Magufuli ni tofauti na uhalisia usiku walitaka kwenda kufungua yale makontena waweke matrekta na magari ili nionekane nilikuwa nadanganya naleta vifaa vya walimu kumbe naleta vya kwangu,” alisema.

Makonda, alisema kulikuwa na wanajeshi wanalinda makinikia ambao wapo chini ya Jenerali Mabeyo walivyowakuta wakaogopa.

“Mabeyo akaweka ngumu hakuna kufunguliwa makontena. Hiyo ilikuwa salama yangu hizi nia njema zina nyakati ngumu sana... halafu huku nimeshatangazwa huyo mkwepa kodi, fisadi anataka kujitafutia mali,”alisema Makonda na kuongeza kuwa:

“Mimi ni mmoja wa wahanga wa haya mambo ya ufadhili Dar es Salaam nilifanya ile kazi ya ujenzi wa ofisi za nyumba za walimu kwa nguvu kubwa nikaomba wadau wa malori, watu wa vituo vya mafuta wakatoa mafuta, Magereza wakatoa watu, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakatoa vifaa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakatupatia askari tukaanza kujenga ofisi za walimu.”

Alisema wakapatikana watu wengine wema kutoka nchini Marekani walijitolea kontena 20 zilizokuwa na thamani. “Zikaingia siasa pale zilikuwa siasa kali kweli kweli, kumbe kuna jamaa wanasema huyu akiendelea hivi na walimu wakimpenda atatusumbua mbele ya safari,”alisema Makonda.

Alisema wakati anapambana kuleta maendeleo kwa walimu wakae katika ofisi nzuri na kuheshimika kumbe kuna baadhi wanawaza tofauti.

“Nilipigwa fitina ambayo sijawahi kuiona duniani ikafika mahali nikasema sasa watajua Mungu yupo ama hayupo. Nikasema hata wakitafuta wateja hawatauza na atakayenunua atalaaniwa yeye na kizazi chake,” alisema.

Makonda, alisema anakumbuka wakati ule bosi wake alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, aliandika barua na kuelezea msaada huo, ilishindikana na kuendelea kushikiliwa kooni.

“Njemba zimekaa vikao vya usiku wakati huo sikuwa najua yale maombi ya kusambaratisha vikao vya sirini kwa sasa nimeshayajua sasa ninawakung’uta na vikao vyao vya usiku wanavyovifanya,” alisema.

Alisema anaelewa asasi za kiraia zinapata changamoto sio kwa sababu wanaleta vitu kwa ajili ya kuuza bali wengine ni kuoneana wivu.

Alisema kulikuwa na upungufu wa vifaa kwa ofisi za walimu zaidi ya 400 wanakaa chini ya miti, aliomba wadau, hajatumia fedha ya Serikali, mtu mmoja anaungana na mwenzake kuharibu.

“Umoja wa waovu huwa haudumu, wanasambaratika tukikutana wananiambia mheshimiwa vipi nawambia kwa neema nimerudi wewe je? Utasika kwa kweli unatutia moyo sana, tukikutazama,” alisema Makonda.

Alisema kuna mmoja alikutana naye kwenye kahawa akamueleza wao ni wale wa Magufuli wanaonewa. “Nikamuambia acha uongo haukuwa wa Magufuli acha unafiki wewe yaani mtu anataka kutengeneza chuki kama una sifa zako utafanya kazi kama hauna sifa hautafanya kazi,” alisema.
Unajua mimi hiki kitu kiliwahi kunishangaza sana kwamba Waziri wa Fedha anamjia juu Mkuu wa Mkoa hadharani wakati wote wawili wapo kwenye Seriukali? Hawa viongozi halishindwa nini kuongea wakiwa wawili ofisini?
Haya maelezo yanaweza kuwa yako sahihi
 
Screenshot_20231102_120808_Remix.png
 
Unajua mimi hiki kitu kiliwahi kunishangaza sana kwamba Waziri wa Fedha anamjia juu Mkuu wa Mkoa hadharani wakati wote wawili wapo kwenye Seriukali? hawa viongozi halishindwa nini kuongea wakiwa wawili ofisini?
Haya maelezo yanaweza kuwa yako sahihi
Kukwepa kodi ni kosa kisheria,kama kiongozi wa umma kuna taratibu za kufuata kabla hujaagiza ili upate msamaha, taratibu hujafuata na wewe ni kiongozi unatakiwa uwe mfano, waziri mpango alisimamia sheria ya ushuru na forodha, huyo RC makonda anacheza na akili na za mazezeta ndo maana mpaka analeta kuna maombi ya kuvuruga vikao usiku,
 
Mimi naongelea approach ya namna walivyoli-epose swala lao kwa umma. Kama Mkonda hakujua taratibu za uagizaji, alitakiwa aelimishwe kabla hajaqgiza. Kwa nini asubiriwe hadi vifaa viwasili nchini kwanza halafu ndiyo mgogoro uanze?

Kwa sababu kwa sasa mimi ukiniambia kuwa hzi zilikuwa ni hujuma kwa Makonda ninakubali

Hii nchi kuna shida mahali fulani
 
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesimulia namna alivyookolewa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo katika sakata la makontena ya vifaa vya ofisi za walimu wa Dar es Salaam kwa kuwa kuna watu walitaka kumchomekea matrekta na magari kwenye makontena hayo.

Makonda aliyasema hayo jana jijini hapa alipokutana na wadau wa mashirika na asasi za kiraia kujadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo changamoto zinazowakabili.

Alisema pona yake ni Jenerali Mabeyo kuzuia makontena yasifunguliwe na ulinzi kuendelea kuimarika, la sivyo matrekta na magari yangewekwa katika makontena hayo ili ionekane hakuleta thamani bali ni magari yake.

“Kipindi kile namshukuru Mungu baada ya kugundua taarifa walizozipeleka kwa Rais John Magufuli ni tofauti na uhalisia usiku walitaka kwenda kufungua yale makontena waweke matrekta na magari ili nionekane nilikuwa nadanganya naleta vifaa vya walimu kumbe naleta vya kwangu,” alisema.

Makonda, alisema kulikuwa na wanajeshi wanalinda makinikia ambao wapo chini ya Jenerali Mabeyo walivyowakuta wakaogopa.

“Mabeyo akaweka ngumu hakuna kufunguliwa makontena. Hiyo ilikuwa salama yangu hizi nia njema zina nyakati ngumu sana... halafu huku nimeshatangazwa huyo mkwepa kodi, fisadi anataka kujitafutia mali,”alisema Makonda na kuongeza kuwa:

“Mimi ni mmoja wa wahanga wa haya mambo ya ufadhili Dar es Salaam nilifanya ile kazi ya ujenzi wa ofisi za nyumba za walimu kwa nguvu kubwa nikaomba wadau wa malori, watu wa vituo vya mafuta wakatoa mafuta, Magereza wakatoa watu, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakatoa vifaa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakatupatia askari tukaanza kujenga ofisi za walimu.”

Alisema wakapatikana watu wengine wema kutoka nchini Marekani walijitolea kontena 20 zilizokuwa na thamani. “Zikaingia siasa pale zilikuwa siasa kali kweli kweli, kumbe kuna jamaa wanasema huyu akiendelea hivi na walimu wakimpenda atatusumbua mbele ya safari,”alisema Makonda.

Alisema wakati anapambana kuleta maendeleo kwa walimu wakae katika ofisi nzuri na kuheshimika kumbe kuna baadhi wanawaza tofauti.

“Nilipigwa fitina ambayo sijawahi kuiona duniani ikafika mahali nikasema sasa watajua Mungu yupo ama hayupo. Nikasema hata wakitafuta wateja hawatauza na atakayenunua atalaaniwa yeye na kizazi chake,” alisema.

Makonda, alisema anakumbuka wakati ule bosi wake alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, aliandika barua na kuelezea msaada huo, ilishindikana na kuendelea kushikiliwa kooni.

“Njemba zimekaa vikao vya usiku wakati huo sikuwa najua yale maombi ya kusambaratisha vikao vya sirini kwa sasa nimeshayajua sasa ninawakung’uta na vikao vyao vya usiku wanavyovifanya,” alisema.

Alisema anaelewa asasi za kiraia zinapata changamoto sio kwa sababu wanaleta vitu kwa ajili ya kuuza bali wengine ni kuoneana wivu.

Alisema kulikuwa na upungufu wa vifaa kwa ofisi za walimu zaidi ya 400 wanakaa chini ya miti, aliomba wadau, hajatumia fedha ya Serikali, mtu mmoja anaungana na mwenzake kuharibu.

“Umoja wa waovu huwa haudumu, wanasambaratika tukikutana wananiambia mheshimiwa vipi nawambia kwa neema nimerudi wewe je? Utasika kwa kweli unatutia moyo sana, tukikutazama,” alisema Makonda.

Alisema kuna mmoja alikutana naye kwenye kahawa akamueleza wao ni wale wa Magufuli wanaonewa. “Nikamuambia acha uongo haukuwa wa Magufuli acha unafiki wewe yaani mtu anataka kutengeneza chuki kama una sifa zako utafanya kazi kama hauna sifa hautafanya kazi,” alisema.
= samani

Siyo "thamani". Samani ni fanicha, thamani ni "value".
 
Mimi naongelea approach ya namna walivyoli-epose swala lao kwa umma. Kama Mkonda hakujua taratibu za uagizaji, alitakiwa aelimishwe kabla hajaqgiza. Kwa nini asubiriwe hadi vifaa viwasili nchini kwanza halafu ndiyo mgogoro uanze?

Kwa sababu kwa sasa mimi ukiniambia kuwa hzi zilikuwa ni hujuma kwa Makonda ninakubali

Hii nchi kuna shida mahali fulani
Maombi ya misamaa ya kodi barua huwa zinaanzia kwa mkuu wa wilaya inapenya hadi kwa rc , alikua anajua taratibu zote,
 
Sijui kama Makonda anaelewa madhara ya kauli yake kwa baadhi ya watu
CDF anaingiaje katika makontena na si Waziri, IGP au Waziri Mkuu?

Ina maana kulikuwa na mawasiliano kati ya CDF na RC na sakata likamlizwa Ikulu 'kiutu' uzima.
Wale wanaotuhumu awamu ya mwendazake hawajapata neno hapa?
 
Back
Top Bottom