johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mkuu wa Mkoa wa Arusha mh Paul Makonda amemuagiza DC wa Monduli kuhakikisha Watumishi 8 wa Halmashauri wanarejesha Fedha walizoiba tsh million 52 Ndani ya saa 24 na kisha wachukuliwe hatua zote za kisheria
Makonda amesema Mwizi ni Mwizi tu awe wa mitaani au Serikalini hivyo Hakuna kuoneana aibu
===
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amembana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Happiness Raphael Laizer, kwa kumtaka kueleza kuhusu hatua zilizochukuliwa baada ya Watumishi wanane kudaiwa kuiba fedha za Halmashauri kiasi cha Tsh Milioni 52.
Akiongea Wilayani Monduli leo May 27,2024, Makonda amesema “Kuna Watumishi wanane wamesepa na Tsh milioni 52 za Halmashauri nataka kujua wapo wapi na hatua gani zimechukuliwa”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli Happiness Raphael Laizer , amesema kuwa Watumishi hao waliwaita kwenye kikao na kuwapa muda wa kulipa fedha hizo ambapo kama hawatalipa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ambapo amesema wametoa muda wa wiki moja fedha hizo kurudishwa.
Baada ya Majibu hayo, RC Makonda alionesha kutoridhishwa na hatua hizo kwakuwa Mwananchi wa kawaida akiiba pesa huchukuliwa hatua kwa haraka za kukamatwa “Ingekuwa Mwananchi wa kawadia hajalipa tu ushuru unakuta mnaenda mnafunga hadi duka lake sasa kwanini Mwananchi hamumpi muda lakini walioiba fedha za Serikali mnawapa muda”
“Watumishi wezi lazima moto uwawakie, lazima tuwapelekee moto kwelikweli, Mwananchi akikosea kidogo anaweza akanyang’anywa hadi samaki na ng’ombe wake (biashara) halafu Mtumishi wa Umma anachukua fedha za Serikali mnaanza kuwapa muda, haiwezekani”
Source: Ayo TV