Makonda ataka watumishi wa Monduli waliokwapua milioni 52 kupitia mashine za POS wapelekewe moto kwelikweli

Makonda ataka watumishi wa Monduli waliokwapua milioni 52 kupitia mashine za POS wapelekewe moto kwelikweli

Mkuu wa Mkoa wa Arusha mh Paul Makonda amemuagiza DC wa Monduli kuhakikisha Watumishi 8 wa Halmashauri wanarejesha Fedha walizoiba tsh million 52 Ndani ya saa 24 na kisha wachukuliwe hatua zote za kisheria

Makonda amesema Mwizi ni Mwizi tu awe wa mitaani au Serikalini hivyo Hakuna kuoneana aibu
===
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amembana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Happiness Raphael Laizer, kwa kumtaka kueleza kuhusu hatua zilizochukuliwa baada ya Watumishi wanane kudaiwa kuiba fedha za Halmashauri kiasi cha Tsh Milioni 52.

Akiongea Wilayani Monduli leo May 27,2024, Makonda amesema “Kuna Watumishi wanane wamesepa na Tsh milioni 52 za Halmashauri nataka kujua wapo wapi na hatua gani zimechukuliwa”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli Happiness Raphael Laizer , amesema kuwa Watumishi hao waliwaita kwenye kikao na kuwapa muda wa kulipa fedha hizo ambapo kama hawatalipa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ambapo amesema wametoa muda wa wiki moja fedha hizo kurudishwa.

Baada ya Majibu hayo, RC Makonda alionesha kutoridhishwa na hatua hizo kwakuwa Mwananchi wa kawaida akiiba pesa huchukuliwa hatua kwa haraka za kukamatwa “Ingekuwa Mwananchi wa kawadia hajalipa tu ushuru unakuta mnaenda mnafunga hadi duka lake sasa kwanini Mwananchi hamumpi muda lakini walioiba fedha za Serikali mnawapa muda”

“Watumishi wezi lazima moto uwawakie, lazima tuwapelekee moto kwelikweli, Mwananchi akikosea kidogo anaweza akanyang’anywa hadi samaki na ng’ombe wake (biashara) halafu Mtumishi wa Umma anachukua fedha za Serikali mnaanza kuwapa muda, haiwezekani”

Source: Ayo TV
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha mh Paul Makonda amemuagiza DC wa Monduli kuhakikisha Watumishi 8 wa Halmashauri wanarejesha Fedha walizoiba tsh million 52 Ndani ya saa 24 na kisha wachukuliwe hatua zote za kisheria

Makonda amesema Mwizi ni Mwizi tu awe wa mitaani au Serikalini hivyo Hakuna kuoneana aibu

Source: Ayo TV
Hivi Makonda kuna vijana anawalipa kumpayusha kwenye social media kwasbb kila sehemu unakuta nyuzi zake anataka kumpiku hata Boss wake Raisi, CCM jitahadhari na huyu kijana mapema samaki hukunja...........
 
Kinachoripotiwa ni Kazi njema za Makonda siyo yeye binafsi.😂😂
 
Kwani wakuu wa mikoa wote 27 hawafanyi kazi nzuri mbona hawalipotiwi, kuna agenda ya siri inao pikwa na wafuasi wake CCM huyu mtu atawasumbua sana kuengua jina lake wakati ukifika 2025 au 2030
Umeshasikia kuna Mkuu wa Mkoa anaenda kuibua Uozo wa halmashauri?

RC anamtegemea DED wanawe waende English medium School 😂😂
 
Mrithi wa magufuli kapatikana.. Ni Habari njema sana ila na yeye katolea wapi magari ya million 500 wakati ni mtumishi
kama wabunge wapayukaji wanamagari ya zaidi ya hyo ije kuwa kwake!!!It doesn't matter what he owns or what as long as he catches a fish!
 
Mrithi wa magufuli kapatikana.. Ni Habari njema sana ila na yeye katolea wapi magari ya million 500 wakati ni mtumishi
Magufuli was a mistake kubwa aliofanywa na CCM huwezi kumpa devil kusimamia nyumba ya malaika......sidhani kama hilo kosa wako tayari kulifanya tena
 
Milioni 52÷8=6.5
Wajinga Sana hao. Wafungwe tu.
Milioni 6 ukimpa mchepuko mbili, ukampa wife laki tano, ukasafisha jina kwa milioni mbili.
Kinachobaki labda ununue pikipiki.
 
Njaa za kijinga sana.

Vijipesa vichache lakini mafisi hawaachi kitu. Hata shilingi mia anakwapua!

Sijui ni ugonjwa wa akili? Wanasaikolojia watusaidie!
Wizi ni tabia na sio kila wizi unasababishwa na njaa,
Mwizi hua hana hela ndogo kwake,
Mwizi anaweza kua na milioni moja mfukoni ila akaiba buku 10 kwa wakati huo.
 
Back
Top Bottom