Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA

Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali

Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda

"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda

Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake

Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam

Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia
Mmmmmmmmh
 
Mungu amsamehe hajui atendalo. Akae alee kichanga chake nasikia anmtoto sasa
 
Pole Mzee Makonda, Nchi inaendeshwa kwa taratibu katiba sheria na kanuni. Aliyekufundisha kuvunja sheria akikuruka ujue kufuata sheeria simpo kama kulia wakati wa ibada kwa askofu
 
Back
Top Bottom