GE2025 Makonda atua kwa Mafundi Gereji Kuomba kura kwa Rais Samia, waahidi Mitano tena

GE2025 Makonda atua kwa Mafundi Gereji Kuomba kura kwa Rais Samia, waahidi Mitano tena

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, ameendelea na kampeni ndani ya jimbo hilo ambapo alikutana na Umoja wa Mafundi wa Suye Garage, ambapo aliwahimiza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025

Akizungumza na mafundi hao waliojitokeza kwa wingi, Makonda alieleza kuwa uchaguzi ni fursa ya kidemokrasia inayowapa wananchi nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa kipindi cha miaka mitano, kwa mujibu wa Katiba

Alisisitiza kuwa miaka hiyo si tu ya kujenga barabara, maji au shule, bali pia ni muda wa kuweka sera, sheria na kanuni zitakazowawezesha watu kuishi kwa amani na maendeleo

Makonda aliwataka mafundi hao kutumia haki yao ya kupiga kura kwa busara na kuwahimiza kuchagua viongozi wenye uwezo wa kutatua changamoto zao

Aidha, aliwaomba kumchagua Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na kumchagua yeye kama Mbunge wa Arusha Mjini na wagombea wa Udiwani kutoka CCM

Kwa upande wao, Umoja wa Mafundi wa Suye Garage waliahidi kumuunga mkono kwa asilimia mia moja pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu


 
Paul Makonda, anajimaliza kisiasa pasipokujua. Mwisho wa siku atajikuta haaminiki.
 
Back
Top Bottom