Makonda: CHADEMA wamekimbia kufanya mikutano na kuanza kulilia vyombo vya habari kufanyiwa mahojiano

huyu jamaa sijui akili yake ina fangasi. yeye hapo ni kibari kipi anacho tumia .ccm ilishakubari chadema wafanye mikutano kama anavyo fanya yeye ovyo kwa kutumia pesa za serikali
Kwanini mnalilia na kung'ang'ania kwenye ofisi za watu kutaka interview? Kwanini msifungue Tv zenu? Pesa za Ruzuku si mnatafuna zote kama mafisi? Mna mchango gani kwenye Tv ile? Mmewahi kuwalipia kodi au bili za maji au umeme au mishahara? Kwanini mnakuwa na akili ndogo kiasi hicho ninyi CHADEMA? Kwanini mnajidhalilisha kiasi hicho?
 
una kumbukumbu au umesahau kama kawaida yako ccm.mara ngapi tunakataliwa au mpaka tuombe tena order kutoka juu
 
una kumbukumbu au umesahau kama kawaida yako ccm.mara ngapi tunakataliwa au mpaka tuombe tena order kutoka juu
CCM tuna Vyombo vyetu vya habari na hatuwezi kuanza kulilia vyombo vya habari visivyo vyetu kama wafanyavyo CHADEMA.
 
Hivi ulisoma shule ya wapi wewe? Unatakiwa ujibu hoja kwa hoja na siyo umekamatwa kwa wizi unaulizwa kwanini umeiba halafu wewe unaanza kusema mbona hata fulani aliibaga? Ndivyo ulivyofundishwa ujengaji wa hoja huo?
Ndo maana Walatin wanasema;
"Ubi praeiudicium regnat, veritas exulat." Yaani kwa lugha rahisi "Animus pollutus caligo est oculis" au kuku rahisishia "Quum animus inquinatur, oculi videre nequeunt"

Yaani "When the mind is polluted the eyes cant see"... Au "The Eyes cant see what the mind already Denied it"

Sasa Nisikilize;

Sijui hata kama unajua Nini maana Ya hoja...
Hakuna Mtu aliyelilia Publicity kutoka kwa Chama Cha wenzetu wa CDM..

Umewahi kujiuliza kama hali ikiachwa hivi na kwa bahati mbaya CDM wakachukua nchi (japo hili siliombei lipitie mbali kabisa)..
Hawawezi kutumia Upuuzi huu huu kuziba maoni Ya raia Wengine?

Lissu alienda kuuliza kuhusu haki yake Ya kikatiba inayolindwa na Katiba ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13 na ibara Ndogo ya 4 na 5 ikilindwa na sheria namba 7 ya mwaka 1994 Kifungu cha 8 kifungu kidogo cha 1 [k]..

Kuhusu Ubaguzi kutoka na Itiqadi na Haiba yake ya kisiasa


Pia nikukumbushe (Kama unajua lakini)
Sheria namba 1 ya 2005 ibara ya 5 inayolindwa na Katiba Ya Tanzania ibara ya 18 kuhusu Uhuru wa Maoni..
Kila mtu anayohaki ya kueleza na kutoa fikra zake kwenye chombo chochote cha Taarifa..


Kama Tunataka Kujenga Taifa la watu wasio kuwa na Elimu wala Uthubutu wa Kuisimamia Katiba na sheria za nchi na kufata matakwa Yao hapo nitakubali ila kama tunataka kujenga Taifa la watu wanaofata Katiba na uthubutu..
Then lissu Yuko sawa..

Sasa sioni Huu uzii wako ulioandika kama una maana yoyote vinginevyo unajaribu kushawishi watu kutokufata katiba..

Na hilo ni kosa la jinai Nikukumbushe tu
Na hii iende kwako na kwa Ujamaa ni mhimu
 
Kwani ukiitwa na kupewa taarifa katika chombo cha habari kufanyiwa mahojiano halafu baadaye siku moja kabla ukapewa taarifa kuwa bwana tunapenda kukutaarifu kuwa kipindi tulichotaka kufanya na wewe mahojiano na wewe tumeahirisha na kwamba tutakutafuta wakati mwingine tutakapoandaa .kuna sababu gani uanze kulazimisha kwenda kuvamia ofisi za watu na kuharibu ratiba za watu? Kwani ni lazima yeye kwenda kuhojiwa?

Niambie kuwa ni kifungu kipi cha katiba wangekuwa wamevunja kama wasingemwita Lissu kwenda kufanya mahojiano naye?

Niambie ni kifungu kipi cha katiba wamevunja kama walimwita kwenye mahot na baadaye wakampatia taarifa ya kuahirishwa kwa mahojiano? Acheni kulazimisha vitu.tumieni busara na weledi. Acheni kudanganyana na kupotoshana. Kila haki ina wajibu wake. Wajibu ni pamoja na kusikiliza maelekezo.sasa wewe unapewa maelekezo na maelezo halafu wewe unaanza makelele yako mitandaoni na kuvamia ofisi za watu utafikiri nyumbani kwako.

Fungueni Tv zenu kama mnataka kuonekana sana kwenye tv.si mmepewa mamilioni kwa mamilioni ya pesa kama Ruzuku?
 
Umeandika mambo makubwa...
HAWEZI KUELEWA...
 

CHAWA kazini ..... una muda kweli.
 
Umeandika mambo makubwa...
HAWEZI KUELEWA...
Hakuna mambo makubwa yoyote ile aliyoyaandika hapo.hakuna haki isiyo na wajibu. Wajibu ni pamoja na kusikiliza maelekezo na maelezo.sasa wewe umeelekezwa jambo halafu wewe unaanza kwenda kuvamia ofisi za watu kutaka uhojiwe. Kwani ni lazima? Kifungu kipi cha katiba kimevunjwa kwa yeye kupewa taarifa ya kuahirishwa kwa mahojiano? Kifungu kipi cha katiba kingekuwa kimevunjwa ikiwa asiingeitwa?
 
Utamuungaje mkono mtu anayesoma kitabu kwa kuangalia kava tu? Ndivyo ulivyofundishwa shuleni?
Shida yako ni kudhani wasomaji hawaelewi, unawaletea habari mpya na za kuvutia!!!
Usipotaja chadema huna habari...
Una sifu-huna habari za uchambuzi...
Mwisho namba ya simu.....
 
Angalau leo umeongea point kuliko siku zote
 

Hivi kwanini mtu ukiwa chawa mpaka akili zako nazo zinakuwa kama chawa mdudu?

Umesikia kauli ya serikali?

Unadhan ingekuwa hivyo unavyodhania ww serikali ingetoa majibu?
 
Kwanza narudia Tena kukwambia hili nadhani ni mara ya Kumi kama sikosei na ni kila siku..

Mimi sio CDM ni CCM mwenye misimamo hai na halisi na ya kisheria Kama Marehemu Mwanangu Ole Mushi..

Kuitwa Kufanya Interview baadae kusitisha kwa kigezo cha kuwa "Tumepata Maelekezo kutoka Juu"
Wewe hakikutii shaka?

Kwanini Maelekezo ya kiahirisha Interview yatoke Juu..

Hili nimeshalizungumzia kwenye Post ya hapo Juu kuhusu Ubaguzi..

Kuahirisha Kufanya mahojiano yaliyopangwa kwa Wiki Nzima na kuahirishwa masaa machache ni uvunjifu wa Sheria ya Habari na uhariri...

Pia ni uvunjifu wa sheria ya Adhabu ya makosa ya Jinai (Penal code) yaani kujipatia Publicity kutumia mtu..

Watu wote Wapinzani na sisi CCM tulifungua wasafi kusikiliza kuwa Ataongea nini..
Ila tukaishia kuambia kuwa kuna maelezo kutoka juu..
Kasome sheria za Habari Tanzania, Kanuni za uhariri ..
Na sera ya Uhuru wa habari Tanzania
Vitakupa muongozo..
Hata hivyo zaidi kajikite kwenye Sheria ya Defamation utapata ABC kuwa walilofanya wasafi lilikuwa ni kosa la kisheria..

PIA NAKUSHAURI KASIKILIZE HOTUBA YA NAPE NAUYE (Waziri pendwa wa Habari kwa miaka yote)..
Kuhusu Sakata la Lissu na Wasafi jana..
Utapata Jibu
 
Naona unasema kuwa kuna sheria imevunjwa. Basi kama kuna sheria imevunjwa mwambie au mshauri kiongozi wako huyo akafungue kesi.kikubwa nawashaurini ninyi CHADEMA mfungue Tv na redio zenu na siyo kila siku kulalamika tu kama watoto. Kwani nini kinawashinda kufungua Tv na redio zenu? Kwani ni shilingi ngapi mpaka mshindwe kufungua? Si hapa majuzi tu mmetafuna billion 2.7?
 
Hivi kwanini mtu ukiwa chawa mpaka akili zako nazo zinakuwa kama chawa mdudu?

Umesikia kauli ya serikali?

Unadhan ingekuwa hivyo unavyodhania ww serikali ingetoa majibu?
Acheni kulia lia ndugu zangu.fungueni Tv na redio yenu.kwani si mmepokea mamilioni kwa mamilioni ya Ruzuku? Hapa majuzi tu si mmebugia Billion 2.7? Mlishindwa nini kufungua Tv kwa miaka yote? Miaka yote si mmekuwa mnalialia tu? Kwanini hamjawahi kuchukua hatua za kufungua Tv zenu? Mtalialia mpaka lini? Mtang'ang'ania mpaka lini kwenye ofisi za watu ili mfanyiwe mahojiano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…