Pre GE2025 Makonda hana jambo dogo, Ng'ombe zaidi ya 400 za chinjwa Arusha ni mwendo wa kula nyama choma bure

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais na Serikali yake wameamua kucheza na akili za Watu wa Arusha kuelekea Uchaguzi Mkuu, yaani wameona nyama choma ndo mahitaji muhimu ya Wana Arusha, hakika inasikitisha

Vitu vya bure siyo vya kukimbilia!! Vingine vina ahadi za kuzimu. Isije ikawa ni ng'ombe wa majini!! Ukishakula unaweuka, unabakia bila akili, unakuwa kama mwashambwa.
 
Ikiwa ni sehemu ya shamrashamra hizo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeratibu tukio hilo eneo la 'Clock Tower' na kwamba, wakazi wa Arusha watakula nyama choma bila gharama yoyote.
Mbunge amealikwa?
 
Makonda ku raise idadi hiyo ya ng’ombe kidogo sana kwake hata bila kutumia pesa yoyote ya serikali
 
Msituharibie mfungo wetu!!
 
Makafara tu hayo wote mtakaokula.mnaenda kupumbazwa akili
 
Kick ya kuusaka ubunge tu!
 
Acheni njaa na uzwazwa wa kushabikia dezo. Badala ya kula na kusherehekea, tunapaswa kuuliza na kujua namna alivyopata hiyo fedha. Na isitoshe, malipo yake ni nini?
 
Rais na Serikali yake wameamua kucheza na akili za Watu wa Arusha kuelekea Uchaguzi Mkuu, yaani wameona nyama choma ndo mahitaji muhimu ya Wana Arusha, hakika inasikitisha
DAB anataka, kwa udi na uvumba, kuwa mbunge wa Arusha. Anajua akipata ubunge na uwaziri ataupata. SASHA ana imani naye sana ndo maana zaidi ya 500 million zinatumika usiku wa leo.
Akae vizuri, yaliyomkuta kigamboni yasije kujirudia.
 
Sio nyama ya ng'ombe ni nyama ya porini. Acha upotoshaji wa kijinga.
 
DAB anataka, kwa udi na uvumba, kuwa mbunge wa Arusha. Anajua akipata ubunge na uwaziri ataupata. SASHA ana imani naye sana ndo maana zaidi ya 500 million zinatumika usiku wa leo.
Akae vizuri, yaliyomkuta kigamboni yasije kujirudia.
Ndo maana akaweka hii event akiamini itampatia wafuasi wa kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…