MAKONDA: Ikithibitika Harmonize anavuta bangi akamatwe awekwe ndani

MAKONDA: Ikithibitika Harmonize anavuta bangi akamatwe awekwe ndani

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ameagiza mwanamuziki Harmonize achunguzwe baada ya kuonekana akivuta kitu kinachotoa moshi na iwapo itathibitika kuwa bangi atamweka ndani.

Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 31,2019 wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Amesema katika mtandao wa Instagram ameona picha ikimuonyesha Harmonize anayetamba na wimbo Paranawe akivuta kitu hicho hivyo ameomba ichunguzwe kama ni bangi au lah.

Harmonize ambaye yupo nchini Ghana, katika mtandao wa Instagram picha yake ikimuonyesha akivuta kitu kinachotoa moshi.

“Nimemuagiza Gavana wa huko achunguze ile ni bangi au nini na ikigundulika ni bangi atakapotua tu hapa ni pingu na kupelekwa lock up, Vizuri namlea mwenyewe na mtoto anapokosea lazima umshikishe adabu bila kujali unampendaje,” amesema Makonda.

Chanzo: Mwananchi
"Kitu kinachotoa moshi" hivi kama aliweka dawa ya mbu ya kuchoma mdomoni ili kujikinga na mbu wa usoni atasemaje?
 
Bashite hana akili yule.
Yaani anakuja kuwapotezea muda watu kwa maisha ya msanii ya picha zake mitandaoni tena akiwa Ghana.

Angeanza na maelfu ya watanzania waliopo Nairobi, Mombasa, Nakuru, Kisumu wanaokula mirungi asubuhi na mchana tena kwa raha zao na uhuru kabisa.
 
Hata kama ni bangi,
Labda sheria za Ghana zinaruhusu kuvuta bangi?!
Kwa mfano huko Tanzania pombe aina ya gongo ni haramu,lakini huku Mozambique inaruhusiwa kama kawaida
Kweli tembea uone
 
Afu Siku hizi mbona naona ule ukaribu wa harmonize Na hao wenzie kama umepungua vile!Nini tatizo?

Hakuonekana kuguswa Na wenzie kufungiwa kwa maana ya Diamond Na Ryvan
Akaonekana anatumia Kama ile Ni fursa ya kutoka Na ku shine Kama Solo Artist

Si unajua Tena Diamond Ni Mtoto wa Tandale
 
Coming to private affairs DAB failed again...
He is a political leader .. An appointee of the President.

Never there when Harmonize signed a contract with WCB... never there from the bottom hustllin..
Why the hell appear today and try to take control of him


...
Hapa naona UCHAWI.... deep hate laid down.
 
Ntarudi.

And by the way ... Harmonize I stand with YOU.

Don't be afraid.
 
Hata kama ni bangi,
Labda sheria za Ghana zinaruhusu kuvuta bangi?!
Kwa mfano huko Tanzania pombe aina ya gongo ni haramu,lakini huku Mozambique inaruhusiwa kama kawaida
Kweli tembea uone

Hivi ni kutafuta sifa au!??

Au Harmonize bado hana Lawyer!?

Maana this is a Public assault.. Ana fans wengi. Kauli ya DAB inaweza ikamfanya apoteze mashabiki wake.

Amshtaki.
 
Mkuu wa mkoa anasaidia kutoa Ķick tena anahamrisha hadi gavana wa nchi nyingine. Makonda kama Trump vile
 
Nadhani "0" iko kazini. Hii wala haitamsumbua HARMONIZE. Kama Ghana wana sheria Bangi na wakimkamata, watamshitaki huko huko. RC mzima kushinda kwenye instagram za watu kuchunguza vitu kama moshi wa bangi, huo si umbeya? Hayo wanayaweza wenye "0" brain.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani "0" iko kazini. Hii wala haitamsumbua HARMONIZE. Kama Ghana wana sheria Bangi na wakimkamata, watamshitaki huko huko. RC mzima kushinda kwenye instagram za watu kuchunguza vitu kama moshi wa bangi, huo si umbeya? Hayo wanayaweza wenye "0" brain.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sheria ya matumizi ya tumbaku na Hamonize ni over 21 yrs of age.
 
Inabidi na kule Wilaya ya Rombo, wachaga wanaovuka mpaka na kuingia kenya kupata Mirungi then wanarudi makwao nao wakamatiwe hukohuko.
Kuhusu Ghana
Ghana imeshuka hadi nafasi 3 kimataifa mwaka wa 2015 kama nchi ambako Cannabis Sativa, inayojulikana kama India Hemp (marujuani) au Bangi kwa hapa Tanzania, inatumika sana kwa raia wake.Ikumbukwe pia hata Zimbabwe tayari bangi inaruhusiwa na siyo madawa ya kulevya na wanakusanya kodi kama bidhaa nyingine kutoka mashambani.
 
Back
Top Bottom