Ukijaziajazia sana unaweza jikuta umesema yasiyotakiwa kusemwa hadharani au ukaji expose identity yako.
Tanzania tukitaka tuidihibiti biashara ya unga kuna vitu viwili vya kufanya.
1.kuongeza ulinzi kwenye mipaka yetu na njia zote zinazotumika kuingiza na kutoa hii midude kwenda nje.imagine dar es salaam pekee ina bandari bubu 50,border za Tanzania ziko loose kuliko viungo vya siri vya kahaba,achana na bandari bubu tunayo hadi mipaka bubu.Mashine za kukagulia mizigo nazo mbovu sasa unategemea utadhibitije hii biashara.ndani ya wiki hizi mbili ambazo makonda kaunguruma unajua zishaingizwa kilo ngapi za unga na punda wangapi wamepakia ndege ktk airport zetu?.customs nako kumejaa rushwa.unaweza pitisha hata fuvu la binaadamu ukiwa na hongo stahili.
2.Kudhibiti pesa ya unga.Hakuna jambo gumu kwa drug dealers wa nchi zilizoendelea kama kutakatisha pesa zao za faida ya unga na kuziingiza kwenye system.lakini kibongobongo ni rahisi mno.kwa makadirio yangu kila siku guanghzou pekee inatakatisha si chini ya dola 50,000-100,000 za unga na kuziingiza kwenye system ya pesa bongo kiurahisi kabisa.kwa wale wakazi wa diaspora kuna kitu kinaitwa remittance hudama kama inayotolewa na western union na moneygram.sasa huku kuna western union za kienyeji.GSM wanahusika kiasi kikubwa na hili tena walivyomaradhuli wanatuchaji sisi katika kutakatisha fedha zao.
Bongo ni kawaida ya mtu kuwa na pesa isiyo na maelezo yaani mtu anabiashara ya milioni kumi lakini ana mali za milioni 500.na hua hakuna maswali.kwa wenzetu mali zako zinatakiwa kuendana na kipato chako kinachotambuliwa na serikali.
Kwahyo cha msingi ni kudhibiti tu pesa ya unga isiwe inamove freely kama ilivyo hivi sasa.kwa mfano ni ngumu kwa drug dealer wa colombia kuhamisha dola laki moja ya unga kutoka marekani kurudi nchini kwake kuliko dealer wa tanzania kuhamisha faida yake ya dola milioni kutoka china kuja dar es salaam.