OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Tuhuma kuhusu Paul Makonda kughushi vyeti vya elimu zilitajwa sana katika awamu ya tano wakati wa msako wa vyeti feki. Wakapululiwa watumishi walioghushi vyeti lakini Paul Makonda akaachwa licha ya tuhuma kuvurumushwa kila kona.
Nakumbuka rais Magufuli alilazimika kujibu tuhuma zile kibabe sana, kwamba yeye ndio rais hakuna wa kumpangia chochote. Wasomi na wapenda haki tukashangaa sana.
Aliyekoleza zaidi tuhuma hizi ni askofu Gwajima akieleza kwa kina maisha ya shule ya Paul Makonda. Ndipo ikajulikana kwamba kumbe aitwa Albert Bashite 😆😆😆
Sihitaji kuandika ese kueleza hili kwa sababu linajulikana.
Sasa basi,kwa sababu awamu ya 5 tuliufyata. Kwa sababu jinai haifi. Basi mamlaka za elimu na kusimamia sheria zichukue nafasi yao kumwajibisha huyu bwana kwa makosa ya kufoji kama ilivyofanyika kwa wengine.
Kule ushirika ambako alisoma degree wakati vyeti vya awali vya mchongo,mnaonaje mkitangaza kufuta vyeti ya degree vya Paul Makonda?
Mkiacha hiyo kitu ipo siku tutawawajibisha kwa kuacha kuchukua hatua.