Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, ameeleza kuwa kulingana na Ibara ya 5(2) na Ibara ya 3(2) ya mkataba kati ya TFF na Sandaland, pande hizo mbili zilitakiwa kufanya mapitio ya kimkataba kila mwaka, lakini kwa miaka mitatu mfululizo hawajawahi kufanya mapitio hayo.
Makonda amebainisha kuwa kutokufanyika kwa mapitio hayo kumeacha utata mkubwa kuhusu masuala ya kodi (VAT), kwani mkataba haujaweka wazi nani anayepaswa kulipa au kubeba kodi hiyo kwa miaka inayofuata kisheria, jambo linaloathiri uwazi wa mapato ya umma.