Makonda na Drama za Watumishi wa Umma

KM wake atapwaya si muda mrefu
 
Kweli anakosea sana:
Hii itakuwa ni maigizo.

Ziara na Mkutano wa siasa ,maswali yote yanapaswa kujibiwa na wanasiasa wa eneo husika.

Vile vile,mikutano ya kiserikali maswali yanajibiwa na watumishi wa Serikali wa eneo husika.

Bila kujua,Katibu mwenezi,anaionyesha dunia kuwa wanasiasa wa eneo husika wameshindwa kuwakilisha matakwa na mahitaji ya wananchi wanaolalamika,huku akiwatoa "kafara" watumishi wa umma,kwa kuwabebesha lawama za kisiasa,huku akijua yupo katika mkutano wa hadhara wa kisiasa.
Ndio,maana wengi wanaona ni maigizo,kutatua kero na shida za wananchi kwa kuamrisha hadharani.
 
Huelewi mipaka ya viongozi wa chama na utendaji katika utumishi wa umma?. JPM alilikoroga na watu wenye uelewa mdogo wakacopy.

Tatizo la kutoelewa sheria kanuni na taratibu kazini zinapelekea mkanganyiko mkubwa. Inawezekana hata Makonda mwenyewe hajui nini anapaswa kufanya kama mwenezi wa chama. Anadhani na yeye ni kiongozi Serikalini. Kuna siku atamhoji mpaka Mkuu wa Serikali ambaye ni Mwenyekiti pia
 
Ni kweli, kwa umati uliojitokeza Kahama kuja kumlaki, Mwenezi Paul Makonda, mimi mpaka nimeogopa!, amepokelewa kama ile siku Masiha alivyopokelewa anaingia Jerusalem, halafu siku chache baadaye ndio ilawa vile!.
P

Mr P, kwa hiyo huyu ndiye masiha ajaye kwenye ufalme wa nchi hii?
 
Hakuna sheria yoyote anayoijua Makonda, na hata mipaka ya kazi yake kama mwenezi sina hakika kama anaijuwa. Sidhani kama itatokea siku yoyote kiongozi wa serikali au mtendaji awajibishwe kwasababu ya drama na kiki zake zinazoendelea. Alifanikiwa kuwachomea wenzie kipindi cha JPM akiwemo yule Meya wa jiji la dsm, kwa Samia haitajirudia.
 
Mkurugenzi Pangani kaisha liwa kichwa,kupitia hizi ziara unazoziita drama,acha chuki zako mwache kijana Makonda hapigie kazi.
 
Mkurugenzi Pangani kaisha liwa kichwa,kupitia hizi ziara unazoziita drama,acha chuki zako mwache kijana Makonda hapigie kazi.
Huyo wa Pangani alikuwa na makando kando yake binafsi, Makonda kapandia hapohapo.
 
Huyo wa Pangani alikuwa na makando kando yake binafsi, Makonda kapandia hapoh

Huyo wa Pangani alikuwa na makando kando yake binafsi, Makonda kapandia hapohapo.
Sasa hapo unasema nini kama sikuwa na chuki tu Makonda?Umesema hakuna mtendaji anayeweza kuwajibishwa kutokana na drama hizi za Makonda,nikakuambia kuna mkurugenzi Pangani kaisha liwa kichwa,unasema huyo alikuwa na makandokando,hata kama alikuwa na hayo makandokando aliwajibishwa na kupitia hizi ziara unazoziita drama.
 
Inashangaza, hata Katibu Mkuu Kiongozi hajawahi kufanya hivyo; wala Makatibu Wakuu wa Wizara hawajawahi kufanya hivyo. Eti Wakuu wa Mikoa, Ma-RPC, Ma-RAS, Ma-DAS na Wakurugenzi, wote 'wameufyata' kwa kijamaa kidogo kwa kivuli cha uenezi. Nilitamani kuona Makonda akieneza itikadi za chama chake, maana wengi hatuelewi CCM ni chama cha mlengo gani. Na pengine atoe mafunzo ili kuongeza wanachama; sasa anafanya kazi za kudozoa na kusogoa bila hata kupata suluhu, na wananchi tumeingia mkenge tukidhani ni malaika kashushwa na roho ya mwendazake. Acha wajinga tuliwe, na baada ya uchaguzi watutafune!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…