DOKEZO Makonda na 'kampeni za kifahari' kuliko wagombea wengine wa CCM, Je, anatuma ujumbe gani?

DOKEZO Makonda na 'kampeni za kifahari' kuliko wagombea wengine wa CCM, Je, anatuma ujumbe gani?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea na kampeni katika mikoa mbalimbali, na kwa sasa wametia mguu wao huku Kanda ya Ziwa.

Ukiachana na mambo kadhaa yanayoacha tafakuri kuhusu mwenendo mzima wa kampeni, yapo mambo mawili yanayonifanya nijikune kichwa, kama siyo kushika tama.

UKWASI WA MAKONDA KWENYE KAMPENI

Paul Makonda ambaye ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, amefanya shughuli nyingi zinazoashiria matumizi makubwa ya fedha. Mfano, kabla ya Rais Samia ambaye ni Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM kufika Arusha, hekaheka nyingi zilizohusisha matumizi makubwa ya fedha zilikuwa tayari zimeanza kufanyika.

Tunakumbuka CCM ilichangisha kupata fedha za Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025, sasa kama ni hizohizo fedha ndio zinatumika, kwa maana fungu lake limetoka CCM, mbona maeneo mengine hatuoni hekaheka za gharama zinazotumika hata nusu ya kile anachotumia Makonda na timu yake!

Kuonesha ukwasi katika mazingira ambayo baadhi ya watu hawapati hata milo miwili kwa siku kunaibua maswali fikirishi, hasa pale kiongozi anapokuwa anaomba nafasi ya uwakilishi. Je, kiongozi wa namna hii anaweza kuwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi?
 
Bashite ashukuru Mungu chadema haijatia team kwenye 'uchafuzi' mkuu mwaka huu...hizo hela zake zingeliwa na ubunge asingeupata!!.
 
Back
Top Bottom