Makonda ni kama hamtaki Mwana FA pale Wizarani

Mwenye akili n threat kwa mpumbavu, muhimu kujua hilo

Kuna nyimbo MwanaFA ametoa unaitwa Baraka Nyingi na Kuna mstari Mmoja upo kwenye huo wimbo unasema SIKUHIZI SIFUMBUI MDOMO, SO SIINGIZI SHOTI...na pia kwenye huo huo wimbo Kuna mstari unasema THESE MOTHER****S NEVER LOVED US.

Hii nyimbo ni kama Ujumbe kwa Boss wake ni kijembe Fulani...na Ile Chorus ya USINIPIME UTAVUNJA HUO MZANI...Ina maana MGUSE AKIWASHE NA MWANAFA ni mtoto wa Tanga Uchawi ulipozaliwa asipodondoshwa mtu Mwaka huu...sijui.

Yetu Tusubiri, Wazee wa Muheza hawatokubali Kijana wao atemwe kijinga jinga watafanya jambo lazima tu
 
Kama hadi wewe unamsema DAB, kweli jamaa atakuwa na damu ya kunguni. Waandishi wa habari mnataka mkae na waziri ili mwende sawa😀😭!!

Tasnia yenu bila kukaa na waziri haiendi? Sawa mnayoitaka ni ipi? Muwe mnafumbia macho habari za serikali kwa kuwa mmepewa bahasha kwenye kikao cha kuwekana sawa??

Yaani waziri wa sheria akutane na wanasheria wote na wajadiliane ili waende sawa, waziri wa ujenzi akutane na wahandisi wawekane sawa, waziri wa maji akutane na wananchi wote watumia maji ili wawekane sawa, waziri wa afya akutane na manesi na kuwekana sawa😆😂😂
 

Brother P, nimekubali hata Mimi naona Boss Kubwa akiwekwa pembeni na huyu wa Muheza akipandishwa kwenye kiti cha Mfalme
 
MWANAFA ni mtoto wa Tanga Uchawi ulipozaliwa asipodondoshwa mtu Mwaka huu...sijui.

Yetu Tusubiri, Wazee wa Muheza hawatokubali Kijana wao atemwe kijinga jinga watafanya jambo lazima tu
Bosi wake ni mpakwa mafuta wa Bwana, analindwa kwa damu ya Yesu, hivyo huo utakuwa mpambano utakuwa wa nani zaidi kati ya nguvu za mwanga na nguvu za giza!.
Najua unajua nani atashinda!, dogo anang'oka!.
P
 
Kama hadi wewe unamsema DAB, kweli jamaa atakuwa na damu ya kunguni. Waandishi wa habari mnataka mkae na waziri ili mwende sawa😀😭!!
Hapa hatumzungumzii DAB huyo ni fictitious being, hapa ni tunamzungumzia bosi wetu PCM na sio tunamsema, kumsema ni mambo ya umbea, hapa tunamzungumzia!.
Tasnia yenu bila kukaa na waziri haiendi? Sawa mnayoitaka ni ipi? Muwe mnafumbia macho habari za serikali kwa kuwa mmepewa bahasha kwenye kikao cha kuwekana sawa??
Kila waziri akiteuliwa mahali, ili afanikiwe ni lazima akae na wadau wake, awape vision yake anataka kuipeleka vipi tasnia katika kipindi chake.

P
 
Hivi watu wa mpira wa chandimu hawana umuhimu kama walivyo wanahabari kwenye wizara hii!?
Nimemuona akitoa kipaumbele kwa rare and isolated sports and games kitu ambacho hakikuwahi kufanyika lakini kina tija kubwa.
Wizara ile ni ajira na sio wizara ya kujichezeshachezesha ili utokee kwenye media.
Anatamani vitu vizuri lakini kuna midubwana inataka kuendelea kunenepesha vitambi na mashavu huku wakiacha viwanja na viunga vya michezo vikijaa buibui.
 
Bashite anategemea zile picha zake alizovujisha na za #1 kujitengenezea uhalali wa kusema chochote na hakuna wa kumhoji hasa huyo mteuzi. Huyu si wanamchekea? basi hebu wamfanye kitu muone jinsi atakavyo hara na kuchafua ukumbi! Bashite anaishi mbele ya muda kwa kutengeneza miskando kisha ana ku blackmail. Muulizeni mtoto wa Moses N. na wa Yusuph M jinsi walivyokuwa Blackmailed.
Ni kuwa tu Jiwe alikuwa alishamstukia mapema na kumtosa pamoja na kufikiriwa yeye ni mshamba, lakini kumbe wa pwani ndio washamba zaidi kwani wao ni wajanja kwenye mipasho tuu na nahau.
 
Yeah yule dogo mwingine ameishiwa ubunifu kabisa akili yake ndio imeishia pale
 
Duh kumbe jamaa ni Mafia anajua kufosi mambo.
Ndio maana nilitaka kushangaa mbona kipindi kile jiwe alimtoa nje ya mfumo halafu karudishwa tena
 
Wale jama Wana UGANGA kinoma siku kuku ALIPO katwa kichwa gafla na kuachiwa

Alilala Chali Huku amelalia mgongo hii DUNIA imebeba mengi
 
Hizi nazo ni voices from within?
 
Bosi wake ni mpakwa mafuta wa Bwana, analindwa kwa damu ya Yesu, hivyo huo utakuwa mpambano utakuwa wa nani zaidi kati ya nguvu za mwanga na nguvu za giza!.
Najua unajua nani atashinda!, dogo anang'oka!.
P
Kiongozi ni nguvu za Giza tu kupambana nani concord zaidi maana kwenye siasa hakuna nguvu ya mwanga, kwamba Bashite analindwa na Yesu??
 
Wale jama Wana UGANGA kinoma siku kuku ALIPO katwa kichwa gafla na kuachiwa

Alilala Chali Huku amelalia mgongo hii DUNIA imebeba mengi
Haya majitu cjui yamechanjia wapi, Mungu atustiri! ni kama Taifa Zima liko chini ya zindiko.. Yale ma mwenge hua yana nini? Watu wa ajabu kina bashite, baba levo, meneja wa diamond wanakuaje viongozi
 
Haya majitu cjui yamechanjia wapi, Mungu atustiri! ni kama Taifa Zima liko chini ya zindiko.. Yale ma mwenge hua yana nini? Watu wa ajabu kina bashite, baba levo, meneja wa diamond wanakuaje viongozi
Mimi na kaka ni role model wangu yupo 55 now
Alisoma vipaji Maalum o- level na advance level

Ana akili ila ana maisha ya kawaida kabisa kabisa

Jamaa ana akili kwenye Baraza la mawaziri hata makamo wa raisi hawafikii uwezo wake

Nawasilisha
 
Mbona mwenyewe nimeogopa
Acha Mimi ni mkristo ila siamini uganga Wala uchawi

Nilipelekwa watu wanajua mpaka kesho CHEZEA WAZIGUA

NILIAMBIWA MAMBO YOTEEEEE HAPA NIPO KWENYE DEBUT NIINGIE HUKO AU NIENDELEE KUISHI KICHWA KICHWA

R.I.P POLE POLE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…