Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Marekani, Omarose Manigault, alifukuzwa kazi kwa matumizi mabaya ya gari la Ikulu ikiwemo kumpeleka na kumrudisha kazini, kitu ambacho hakiruhusiwi USA, imebainika wiki hii.
Unadhani msafara wa harusi na shughuli nzima ya swahiba wa RC utatumia hela ngapi za magari, payroll ya jeshi la polisi, ofisi ya RC, na vyombo vya usalama?
Viongozi wa ki-Afrika wanaishi kwa anasa kwa hela ya walipa kodi. Na walipa kodi wenyewe sisi ni mazuzu tusiojua ya muhimu ya kufuatilia, waandishi wanamuuliza Mkuu wa Mkoa kama atasimamia harusi ya Le Mutuz. Sasa ukiwa unatawala mijitu kama hii kwa kweli unafika mahala unasema labda acha akina Makonda wale jasho letu.
Halafu jana Rais anasema anarudisha Tanzania ya Nyerere. Regional Commissioner wa Nyerere atajinasibu mbele ya waandishi kwamba anaenda simamia harusi ya Le Mutuz? Mtu anaerusha picha zake kutokea bafuni guest house?