Habari Muheshimiwa Makonda! Mimi kwa kweli siwezi kuhukumu mtu pasipo na vithibitisho, ila kwa mwenendo ulivyo na ukimya nina amin kuna asilimia kubwa ya walakini kwenye hili linalosemwa kutokana na kuamua kuwa kimya ......
Kama vyeti hakuna, hemu jitokeze tu na ukiri kukosea (Wengi wametenda kama inavyosemekana umetenda, wewe SIO WAKWANZA), jitokeze tu kiungwana kama mkristo safi, na useme Watanzania wenzangu mimi nilifanya 1,2,3,4 & 5, uwezo wa kuendelea NA KAZI YA UKUU WA MKOA ninao, nisameheni, tusonge mbele, nina uhakika pia utakuwa umemfanyia haki Mkuu wetu.
Ukifanya hivyo mi nina uhakika watu watanyamaza (WATANZANIA NI WATU WAUNGWANA TU) na litakuwa limepita kabisa. Ninajua pia hakuna atakayekusumbua wala nini na utaendelea vyema na kazi njema ambayo kwa sehemu inaonekana, kwa ukweli kwa sasa nakuonea huruma.
Jitihada nyingine zozote unazofanya za kuushawishi umma kuwa unafanya kazi nzuri ni sawa ila unaonyesha tu kuwa upo desperate, huo ndo ukweli. Come out and say something, kanusha au kukubali, it wont even take more than 10 minutes, tutalala, kesho itafika na itakuwa historia.