Wakuu poleni na weekend kavu,
Niende kwenye mada moja kwa moja.Nakumbuka hotuba ya Waziri mkuu aliyelazimishwa kustaafu na mwishowe akakkatwa na hatimaye akaenda kununua Chadema ili agombee uraisi kwa tiket ya ukawa.sikumbuki maneno yote ila kuna sehemu katika hotuba ile alisema,Namnukuu" Naona tatizo ni uwaziri mkuu,naona tatizo ni uwaziri mkuu".Naanza kupata fikra mbaya kwamba hii vita ya vyeti vya Bashite sio tatizo,tatizo ni "DONA".kuna ukakasi ndani ya jambo hili,watu wameacha kufocus kwenye "DONA"wanahangaika na vyeti.mimi sio kada wala mfuasi wa chama chochote hapa TZ,nimemaliza Advanced level 1993 mnaweza kukadiria umri wangu,sijawahi kupiga kura hata mara moja,lakini naona kuna watu wanatuzuga sana tuelekee kwenye vyeti,napata hofu wanahusika na biashara hii ya "SEMBE'.Najiuliza tu peke yangu,sasa hivi" Bashite" akifukuzwa,au akijiondokea tutarudi kujadili "SEMBE" au tutatafuta mtu mwingine ambaye hana vyeti au ana vya uwongo?kwa nn tunafanywa wajinga na watu wachache?badala ya kujadili hoja zote mbili ya" DONA" na "BASHITE",tumevurugwa tunajadili upande mmoja ambao hauna madhara.Tuamnkeni jamani tusipelekwe na Upepo.Ingekuwa ni Upinzani umeanzisha hii vita ya "DONA"afu wana Lumumba wanazungumzia vyeti vya Hamad Rashid watu wangetokwa Povu sana na kusema tunapoteza muda ku discuss petty issues!Sisemi Bashite yupo sawa ila tujadili vyote viwili tu!Tunatumia nguvu nyingi kuzima swala la "SEMBE"badala ya kuhangaikana "Bashite".Au kwa vile Freemasson alitajwa?