Pre GE2025 Makonda: Pesa za mafao ya ubunge tusiwape wajumbe, karibuni kuwekeza Arusha

Pre GE2025 Makonda: Pesa za mafao ya ubunge tusiwape wajumbe, karibuni kuwekeza Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge,uwekezaji wa Umma PIC, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatatu Februari 17, 2025 amewakaribisha wajumbe wa kamati hiyo ambao ni wabunge wa Bunge la Tanzania kutumia mafao yao kwenda kuwekeza Jijini humo, badala ya kutumia Mafao hayo ya Ubunge kwenda kuwapatia wajumbe, ili kuwapitisha kwenye uchaguzi.

Soma Pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akihimiza umuhimu kuwapatia wajumbe wa mikutano ya vyama vya siasa ndoto za kule nchi inapoelekea, maono ya wagombea na mipango ya kuwaondoa wapigakura kwenye mikwamo mbalimbali ikiwemo umaskini, Mhe. Makonda amesema Arusha inazo fursa mbalimbali za kiuwekezaji na ni muhimu kwa Wabunge hao kuweka alama ya utumishi wao wa kibunge kupitia uwekezaji wa maeneo mbalimbali mkoani Arusha ikiwemo sekta ya migahawa na hoteli kutokana na mahitaji makubwa ya huduma hizo.

 
Back
Top Bottom