Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema Maandalizi ya kumpokea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yamekamilika na kueleza kuwa Rais Samia ni Mwanamke wa Mfano duniani hivyo wao kama Mkoa wanajivunia Rais Samia.
Sherehe za Siku ya Wanawake Kitaifa zinatarajiwa kufanyika tarehe 8 siku ya Jumamosi jijini Arusha ambapo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndiye Mgeni rasmi wa shughuli hii.