Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Tuhuma zako ni nyingi sana kuwa umeshiriki utekaji, mateso na hata uuaji. Pengine hizi tuhuma ni kweli au pia sio kweli. Lakini mwenye majibu kamili ni wewe mwenyewe.
Sasa tuambie ukweli, wakati watu wamejawa na mashaka kuwa Roma Mkatoliki ndio ametoweshwa kabisa kama Ben Saanane ulijitokeza na kusema atarejea Jumapili (kama vile alikuwa nyumbani kwako) na kweli alirudi.
Tuambie tena jee kina Saanane na Azory kwa nini nao hawakurudi "Jumapili" kama mwenzao?
Usione tuko kimya tuna majonzi makubwa mno.
Ili hayo yasiibuke tena kwenye hii mikutano ya kisiasa inayoanza tena nakushauri wahi kujibu tuhuma hizo na kama unasingiziwa lakini unaujua ukweli uweke wazi
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app