Makonda: Stendi mpya Iringa ipewe jina la Chongolo

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema ataishawishi Serikali na Uongozi wa juu mara baada ya kukamilika kwa stendi mpya Iringa ili ipewe jina la aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwakuwa ameacha alama ndani ya CCM.

Makonda amenukuliwa akisema “Hapa kuna Kaka yangu Chongolo, nilikuwa nae yeye akiwa Mkuu wa Wilaya MimI nikiwa wa Mkoa Dar es salaam, yeye akiwa Katibu Mkuu wa CCM na mimi nikiwa Mwenezi wake sasa nilivyoambiwa kuna hitajika stendi nami nikasema kwa heshima ya Chongolo basi nami nitalibeba ili tuongeze sauti kuhakikisha tunajenga stendi angalau Mwana Mafinga Chongolo awe sehemu ya kumbukumbu na nitawashawishi Viongozi waweke jina la Chongolo kwenye stendi ikiwa sehemu ya kumbukumbu"

Makonda ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Mafinga Mjini mkoani Iringa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa 20.

Credit - MillardAyo
Puuzi tu kama yule alisema sura ya mtu kuwekwa kwenye noti.
Kwa hiyo wananchi wataneemeka kwa hilo!!
Poyoyo.
 
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema ataishawishi Serikali na Uongozi wa juu mara baada ya kukamilika kwa stendi mpya Iringa ili ipewe jina la aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwakuwa ameacha alama ndani ya CCM.

Makonda amenukuliwa akisema “Hapa kuna Kaka yangu Chongolo, nilikuwa nae yeye akiwa Mkuu wa Wilaya MimI nikiwa wa Mkoa Dar es salaam, yeye akiwa Katibu Mkuu wa CCM na mimi nikiwa Mwenezi wake sasa nilivyoambiwa kuna hitajika stendi nami nikasema kwa heshima ya Chongolo basi nami nitalibeba ili tuongeze sauti kuhakikisha tunajenga stendi angalau Mwana Mafinga Chongolo awe sehemu ya kumbukumbu na nitawashawishi Viongozi waweke jina la Chongolo kwenye stendi ikiwa sehemu ya kumbukumbu"

Makonda ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Mafinga Mjini mkoani Iringa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa 20.

Credit - MillardAyo
Yaani stendi ya IPOGOLO ibadilishwe iitwe jina la CHONGOLO? Kafanya kitu gani chenye matokeo Chanya kuzawadiwa kumbukumbu ya kiwanja?

Kumbukumbu ya jina la mtu aliye hai kupewa sehemu au miundo mbinu yoyote ni kumchuria huyo mtu. Stendi ya IPOGOLO haiwezi kubadilishwa jina na kupewa mtu ambaye wala hakushiriki kwa namna yoyote uanzishaji wake hata Msigwa alikataa kuitwa kwa jina lake ndio maana inatumia jina la eneo husika.
 
Back
Top Bottom