mjanja wa kijiji
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 1,582
- 4,378
alienda kuchukua majukumu ya kocha lakini kaumbuka.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimesikia kauli hii ikitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, kuwa timu ya taifa Taifa Stars ni mali ya Chama cha mapinduzi na kuwa Taifa Stars ikishinda imeshinda CCM. Kauli hizi ni moja ya kauli za hovyo ambazo haziwezi kutolewa na kiongozi mwenye busara anayejua maana ya mpira ni nini.
Kwanza inaondoa umoja na mshikamano kwa wapenzi, mashabiki na wachezaji wenyewe, badala ya michezo kutumika kama njia ya kuliunganisha taifa kauli hizi zinaendeleza mpasuko.
Nawashauri viongozi hasa wa kisiasa wajitahidi kutoingiza siasa kwenye michezo, michezo ni burudani, michezo ni furaha unapoleta siasa kwenye michezo unaharibu maana halisi ya michezo.
Mwisho kabisa napenda Makonda ajue kuwa Taifa Stars ni timu ya watanzania wote wakiwepo wasio na vyama.
Poleni watanzania kwa kufungwa 3-2 na majirani zetu Kenya, next time tutajitahidi nasi tushinde.
View attachment 1140639