Makonda: Taifa Stars ni mali ya CCM

Makonda: Taifa Stars ni mali ya CCM

Baada ya kipigo hiki.atahamia kwa samagoal ufungaji bora kule ughaibuni ni juhudi za awamu ya tano!
 
Nanukuu:
Kuna kiongozi mmoja kijana serikalini hajielewi.
Mwisho wa kunukuu.
 
Siasa kwenye Mpira.....haya bebeni aibu yetu hiyo nyie wavaa maguo ya kijani.
 
Nimesikia kauli hii ikitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, kuwa timu ya taifa Taifa Stars ni mali ya Chama cha mapinduzi na kuwa Taifa Stars ikishinda imeshinda CCM. Kauli hizi ni moja ya kauli za hovyo ambazo haziwezi kutolewa na kiongozi mwenye busara anayejua maana ya mpira ni nini.

Kwanza inaondoa umoja na mshikamano kwa wapenzi, mashabiki na wachezaji wenyewe, badala ya michezo kutumika kama njia ya kuliunganisha taifa kauli hizi zinaendeleza mpasuko.

Nawashauri viongozi hasa wa kisiasa wajitahidi kutoingiza siasa kwenye michezo, michezo ni burudani, michezo ni furaha unapoleta siasa kwenye michezo unaharibu maana halisi ya michezo.

Mwisho kabisa napenda Makonda ajue kuwa Taifa Stars ni timu ya watanzania wote wakiwepo wasio na vyama.

Poleni watanzania kwa kufungwa 3-2 na majirani zetu Kenya, next time tutajitahidi nasi tushinde.

View attachment 1140639
 
Back
Top Bottom