GE2025 Makonda: Tuishi katika Misingi Imara ya Kiroho na maadili mema

GE2025 Makonda: Tuishi katika Misingi Imara ya Kiroho na maadili mema

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, leo ameshiriki ibada maalum na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ngarenaro, lililopo katika Kata ya Ngarenaro, Jimbo la Arusha Mjini. Katika ibada hiyo ya Jumapili, Makonda alipata fursa ya kuzungumza na waumini wa kanisa hilo, ambapo aliwashukuru kwa maombi na ushirikiano wanaoendelea kumpa katika safari yake ya kisiasa na maisha kwa ujumla.

Alitumia nafasi hiyo kuwatakia ibada njema, huku akisisitiza umuhimu wa kumshukuru Mungu kwa kila hatua ya maisha. Akizungumza na waumini hao, Makonda alieleza kuwa moja ya ndoto zake kubwa katika maisha ni kuona jamii inayojengwa katika misingi imara ya kiroho na maadili mema, ambayo yatasaidia kulijenga Taifa lenye mwelekeo sahihi. Katika hotuba yake, Makonda alitoa pendekezo kwa kanisa hilo kuanzisha sikukuu maalum ya kusifu na kuabudu, ambayo itakuwa na lengo la kurejesha heshima ya Makao Makuu ya KKKT yaliyopo ndani ya Jimbo la Arusha Mjini.

Alisema kuwa tukio hilo litakuwa sehemu ya kutangaza Injili ya Kristo, na litakuwa na maana kubwa kwake binafsi kwa kuwa nyimbo za sifa na ibada zimemletea uponyaji na faraja katika maisha yake. Aidha, Makonda alitoa ombi kwa uongozi wa kanisa hilo kuandaa mpango maalum wa mashindano ya watoto kusoma Neno la Mungu, akieleza kuwa mpango huo utawajengea watoto uwezo wa kuelewa na kueleza maandiko kwa ufasaha zaidi.
 
Waache viongozi wa ibada nao wapate chochote kitu cha kuweka mfukoni
 
Back
Top Bottom