Makonda wa Arusha ruti ya Kilombero kwenda Kiseriani Madukani wanaibia abiria nauli

Makonda wa Arusha ruti ya Kilombero kwenda Kiseriani Madukani wanaibia abiria nauli

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Hii ni kero ya watu wengi nimeamua kuiweka hapa ili wahusika wachukuliwe hatua,

Kwanza kabisa kwenye mwezi wa tano hawa jamaa wa haisi walikuwa hawafiki mwisho wa ruti kwa zaidi ya miaka miwili walikuwa wanaishia relini yaani kuna kama km4 hivi ndo ufike kiseriani mafukani, ambapo nauli ilikuwa ni 700 ile ile

Sasa baada ya kuamrishwa kufika mwisho wa ruti wakawa wanafika ikiwa nauli ni hiyo hiyo 700

Kero inakuja ni kwamba abiria ukishukia relini unalipa 600 lakini ukivukishwa tu reli hata mita 100 wao wanakata 700 utake usitake labda tu umpe 600 kamili

Ni kero yangu ya leo mimi siku hizi napanda na 600 yangu sitaki usumbufu.
 
Hii ni kero ya watu wengi nimeamua kuiweka hapa ili wahusika wachukuliwe hatua,

Kwanza kabisa kwenye mwezi wa tano hawa jamaa wa haisi walikuwa hawafiki mwisho wa ruti kwa zaidi ya miaka miwili walikuwa wanaishia relini yaani kuna kama km4 hivi ndo ufike kiseriani madukani, ambapo nauli ilikuwa ni 700 ile ile

Sasa baada ya kuamrishwa kufika mwisho wa ruti wakawa wanafika ikiwa nauli ni hiyo hiyo 700

Kero inakuja ni kwamba abiria ukishukia relini unalipa 600 lakini ukivukishwa tu reli hata mita 100 wao wanakata 700 utake usitake labda tu umpe 600 kamili wakati kitua hadi kituo imeandikwa 600

Ni kero yangu ya leo mimi siku hizi napanda na 600 yangu sitaki usumbufu.
 
Mkiambiwa nunueni vitz/starlet mnasema vigari vya kike hivyo.

Haya sasa
 
Sasa hapo umeibiwa Nini, lipa 700. 600 inaishia relini, ukivuka tu relini ni mwendo wa 700.
 
Wako Sawa Mkuu. Mimi Nawalipa tuu ile barabara kwanza Mbovu Sana Inastahili Lami Kabisa lakini Serikali Yako Imelala haiweki Lami.. kakipande kadogo tu kamewekwa lami Sasa Fikiria Rough Road toka juu ya reli kidogo hadi Round about ya Kiseriani ni mwendo wa kukimbia Nusu Saa kwa miguu na hakuna lami ni Vumbi tuu.

Vipuri vya magari bei juu.

Shukuru hata sasa mia saba tuu unafika kwako.

Serikali iweke lami hii barabara kuu ambayo ni Short cut muhimu kutoka njiro hadi Moshono.
 
Back
Top Bottom