Makonda wa daladala pandisheni nauli za daladala, msiwe wajinga.Mbona wao wamepandisha tena bila kusubiri majadiliano.

Makonda wa daladala pandisheni nauli za daladala, msiwe wajinga.Mbona wao wamepandisha tena bila kusubiri majadiliano.

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Mwishoni mwa mwezi April serikali na wadau wa Usafirishaji na Usafiri walifanya kikao kujadili gharama za Usafirishaji na kufikia makubaliano ya nauli mpya ambazo zingeanza kutumika katikati ya mwezi Mei.

Leo asubuhi nasikia mafuta yamepanda na kuuzwa elfu 3 na ushehe kwa petroli na diesel lakini cha kushangaza daladala leo wanabeba watu kwa nauli ileile ya miaka mingi iliyopita.

Pandisheni nauli haraka.

Kama ni athari za Ukraine & Russia war basi kila mmoja aonje hiyo ladha.

Nje ya mada: Kwanini serikali isiende kununua mafuta Urusi ambako yanauzwa kwa bei ndogo zaidi kuliko nchi zote duniani?.
 
Hatufungamani na upande wowote lakini tunashindwa kununua mafuta Urusi sisi ni nani?

sisi ni wajinga
 
Huna akili, watapandisha vipi wakati walikubali nauli ipande siku ya 14
 
Huna akili, watapandisha vipi wakati walikubali nauli ipande siku ya 14
Na majadiliano ya nauli yalikuwa kwasababu ya bei ya mafuta iliyoanza leo au baada ya kupanda ile mara ya kwanza?

Kama majadiliano yalikuwa kwasababu ya kupanda mafuta mwenzi Machi -Aprili huoni hapo kuna haja ya nauli kupanda kwa dharura kutokana na kupanda bei ya mafuta kwa dharura?
 
Ruhusa ni bei kupanda baada ya siku 14, ukiona chombo hakikupi faida baki subiri tarehe 14
 
Back
Top Bottom