Makonda, wanakutumia kuelekea 2025. Wakizingua gombea mwenyewe

Makonda, wanakutumia kuelekea 2025. Wakizingua gombea mwenyewe

Sina mashaka na upeo na uelewa wako katika hili.

Naamini wewe unaijua vizuri CCM.

Kwa ufupi Sana,Jamaa wamekuweka hapo kutafuta kura za wasukuma. Bahati nzuri kabisa hii ni fursa kwako ya kujitangaza na ilivyo ajabu Watanzania wamekupokea vizuri Sana.

Unaushawishi na kuna maono mazuri uliyaona kutumia jina la magufuli. Hakuna shaka jina lile ni kubwa na ndiye mpinzani mkubwa wa CCM kwasasa.

Makonda, nimekuangalia vizuri na kutafakari juu yako nimeona unakitu chenye matumaini kwa Watanzania. Niweke wazi kwamba Mimi napenda kiongozi yoyote anayetumia muda wake kusikiliza kero za wananchi/watu wenye kipato cha chini na wasio na mamlaka ya kiuongozi.

Na Hawa ndiyo wengi katika nchi yetu. Wewe umekuwa ni msaada mkubwa kwao kwa muda huu wanajaa kwenye mikutano yako kwasasabu wanajua wamepata mkombozi wa kuwasikiliza na kutatua kero zao.

Lakini hiki unachokifanya wapo wanaccm hawafurahii kabisa na wamepandikiza watu wa kukufuatilia kwa ukaribu. Yule Jamaa wa Mtama, mambo ya nje, Madelu, Chalinze na yule RC wa rocky City waogope kama ukoma.

Mimi nasema kwa siku za usoni na kariba yako unawafaa Watanzania na unaifaa Tanzania. Wazee wa mara wamekukabidhi kifimbo kama cha mwalimu Nyerere.

Si jambo dogo kuaminiwa na kufananishwa na mwasisi wetu. Jina lake ni kubwa na mambo yake ni makubwa.

Kama wamekuamini kwa hilo basi wameona kitu kwako. Tambua hawajawahi kufanya hivi kwa kiongozi yyte kwa miaka ya hivi karibuni. Na kusihi kabla hujatoka mara nenda butiama kwa mwalimu kampe heshima yake na upate baraka za mwalimu.

Makonda Mimi huwa naamini katika mtu na si chama. Nimekuona nimekuchambua toka ukiwa DC,RC na sasa itikadi. Wewe ni mmoja wa viongozi wanaoitwa " machinery leaders/governors." Nchi yetu ili isonge inahitaji a no nosense Man.

Tukiwa na kiongozi wa namna hii ndiyo tunapinga RUSHWA na ufisadi,ndiyo tutaepeukana na kasumba ya kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi na ujenzi haufanyiki wananchi wanabaki kusubiri miaka nenda miaka Rudi.

Kama hutabadilika makonda unawafaa Watanzania. Go makonda go plz.

Nakuwekea na haka ka video.
Acha kumfanganya huyo Zerobrain !! Kwanza hana akili za kutawala pili huyu Bashite ni mfungwa mtarajiwa tu. Upende usipende, baada ya Samia kutoka madarakani Makonda atapandishwa mahakamani kwa makosa yenye ushahidi ambao haufutiki.
 
Makonda hana properties za uongozi hata moja, hajui mipaka yake ya kikazi, anafanya mambo kimihemko ni ignorant pekee ndio wanaoweza kumuelewa, "viongozi wanyanyua mabega hawatufai"
::Let's continue watching the game!
🤣🤣🤣
 
Tatizo la masikini na wajinga ni kudhani kiongozi akifokewa hadharani au kukashifiwa ndio utatuzi wa kero zao.
Sio kweli, eti we mkuu wa mkoa jibu hili! Afisa ardhi kwanini kiwanja kile hakupewa yule na kadhalika kama hayo hayana msaada maana ni USANII MTUPU, ona alikopita huyo mwenezi wenu mambo yamebaki kama kawaida labda kaiumbua tuu serikali ya CCM na viongozi wake tuu
Mujukwaa ya "futuhi....."..
 
Makonda hana properties za uongozi hata moja, hajui mipaka yake ya kikazi, anafanya mambo kimihemko ni ignorant pekee ndio wanaoweza kumuelewa, "viongozi wanyanyua mabega hawatufai"
::Let's continue watching the game!
kati ya watu wajnga wewe ni mmoja wapo
 
Huu ushauri ukiutazama haraka ni mzuri ila ni wa kuangamiza mtu mazima ukifuatwa.
 
Nchi km tz inahitaji watu kama makonda maana ukisema sijui ufate mipaka kwa majizi tuliyoyaamini yatuongoza tutaishia kulia tu .Kuna watu wanaonewa hii nchi ww na hawana pa kwenda.Acha hata makonda ajaribu maana watu watapunguza hata hasira kwa kuongea maana wanakufa na mafaili wakitafuta haki zao.
Makonda lenyewe ni jizi, halafu eti nchi ya majizi inahitaji viongozi kama Makonda.
 
kati ya watu wajnga wewe ni mmoja wapo
Hatuwezi kuwa sawa kimitizamo wala hatuwezi kufanana kimitizamo, wewe unaweza kuona kengeza lakini mimi nikaona chongo! Sio muumini wa kiongozi mwenye mihemko na amsha amsha! Nasimama katika principles!
 
Back
Top Bottom