The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amewahimiza wakazi wote wenye sifa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kupiga kura hapo Kesho Jumatano Novemba 27, 2024 ili kuwachagua Viongozi wa serikali za Mitaa watakaoshirikiana na Viongozi wengine kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao.
Makonda ametoa wito huo leo Novemba 26, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha kwenye Soko la Kilombero wakati wa ufanyaji wa usafi kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya upigaji wa kura ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amekwisha tangaza kuwa siku hiyo itakuwa ni mapumziko ili kuwaruhusu wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi huo.
Soma Pia:

- Makonda awaomba viongozi wa dini kuhubiri amani uchaguzi wa serikali za mitaa
- Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024