Makonda: Wanaume wafanyakazi wakatwe asilimia 40 ya mishahara yao wapewe wake zao

Makonda: Wanaume wafanyakazi wakatwe asilimia 40 ya mishahara yao wapewe wake zao

Dadeki!! Hili ni tatizo mtu anapokea laki moja anakatwa na asilimia 40!! Huu ni upuuzi tuuzeni na nchi tugawane hela

Nimekutana na bango kwenye hizi skrini zenu za matangazo barabarani [ADN], muda huo linasomeka “TANZANIA NI TAJIRI”.... kwa hayo machache naunga mkono hoja yako.

Nchi iuzwe tugawane kila mtu afe na chake, maisha yenyewe yako wapi.... mara Corona hii hapa.
 
Kazi si anafanya yeye, hii ni moja ya dhana ya kuwaangamiza wake wanawake, huwezi sema haki sawa halafu ukatengeneza vitu kama hivyo. Kwa hiyo mwanamke akiwa kazini nae akatwe apewe mme wake?

Unadhani hapo ni kuwapa changamoto wanawake watafte pessa au walale tu wakitegemea hella kila mwezi
Upo sahihi mkuu wa mkoa wanaume pesa zao zinaishia kwa mchepuko na bar nakuwasahau wake na watoto wanateseka majumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya kufikirika yasiyotekelezeka, hiyo 40% baada ya makato yote ya kisheria au baada? Je, wale wenye wake wawili watakatwa 80%? Hivi vyeo vingekuwa vinatolewa kwa utaratibu maalumu sio hobela hobela.
 
Wale Waislamu wenzetu waajiriwa wenye wake 3 wakatwe 120%, hiyo 20% iwe mkopo. Hii itasaidia kila mke apate hiyo 40%. Mshahara ni mdogo sana kuwapa 40% wagawane.
Uislamu unafundisha jinsi ya kuishi na wake awe mmoja au wawili au watatu au wanne ni mtu mwenyewe kufuata au kuacha kufuata. Mume ndio msimamizi wa wake
 
Hivi kama mwanamke na mwanamme wote wako sawa kwa nini upendeleo umlenge mwanamke. Nilitegemea kusiwepo upendeleo wa aina yeyote. Ndio maana ya haki sawa.

Inabidi sheria itaje basi kuwa mwanamme yuko juu ya mwanamke then apewe upendeleo kwa sababu hawalingani. Lakini kama mwanamke na mwanamme wanalingana kwanini mwanamke apendelewe kwa kupewa vipaumbele vingi kuliko mwanamme.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom