Makonda: Wanaume wafanyakazi wakatwe asilimia 40 ya mishahara yao wapewe wake zao

Kwa sisi wengine ambao hatuja ajiriwa inakuaje tukiwa na wake zetu mswada wetu utakuaje maana kuna kaubaguzi hapa vile yaani
 
Wakifanya hivi Dkt Mwaka atabaki na asilimia ngapi maana bado ataongeza tena mke😂😂😂
 
He is dangerously stupid...
Ningemuona wa maana sana kama angeweza kusaidia kuongeza ajira za kinamama na wao wajiinue kiuchumi.

Hapa si tu kafanya kosa la kutoongeza uzalishaji (anataka kilichopo kigawanywe badala ya kuongeza uzalishaji), bali pia amewadhalilisha wanawake kuwa ni watu wasioweza kujitafutia wenyewe, mpaka wapewe kilichotafutwa na wanaume.
 
LEO TULIKUWA NA KIKAO KIZITO KWELI KWELI.
SISI TUKIWA MABAHARIA, TUMEFIKIA MAKUBALIANO KWAMBA KIONGOZ WETU ANAUONA MZURI SANA NA TUNAOMBA FIKIRA ZA KIONGOZI ZIDUMU(TUSEME WOTE JAMANI).
KWA HIVYO TUNAKUBALI 40% IKATWE, KAMA ITAMPENDEZA AKATE HATA 60%(MAANA ANAWEZA KWANI YEYE NDIYE MWAJIRI).
Lakini sasa:1.HATA TUKIMGONGA BARMAID MAGETONI TUSISEMWE MAANA 40% TUSHATOA,
2.TUSIULIZWE JUU YA ADABU ZA WATOTO KWANI 40% IPOO
3.TUSIULIZWE AKIPATWA NA MSIBA, MAGONJWA KWANI SI BADO 40% IPO MZEEBABA.
4.WAKWE,NDUGU N.K WASITUJUE KWANI 40% BADO IPOO.
zidumu fikra za kiongizi mtukufu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiweka hiyo 40%,bima ,heslb plus kodi unarudi na mbupu home mwisho wa mwezi
 

The guy is not that bright.

I mean, how does that empower women?

Badala ya kuja na mipango ya kuwainua wanawake, yeye anakuja na upuuzi wa kumfanya mwanamke aendelee kuwa duni na tegemezi kwa mwanaume!

Mwanamke kuendelea kuwa tegemezi kwa mwanaume, hakumuinui hata kidogo.

Aje na mpango wa kutoa mikopo midogo midogo yenye unafuu kwenye riba. Mikopo inayoweza kumsaidia mwanamke kuanzisha walau ka-biashara kake kadogo.

Aje na mipango ya kuwafunza wanawake kazi na kuwafunza biashara zenye manufaa kwao ili wawe na uhuru wa kifedha [financial independence].

Aje na mpango wa kuwafunza wanawake namna ya kuongeza vipato vyao na kuongeza akiba ya fedha.

Aje na mpango wa kuwajengea wanawake self-esteem na kuwafanya wajiamini [confidence].

Katika kufanya hayo, kwa kujua au hata kutojua, atakuwa anatengeneza viongozi katika jamii.

Wasichana wadogo wakikua huku wanaona wanawake wakijifanyia mambo wao wenyewe bila kutegemea wanaume, watakua wakijua kuwa hata wao wanaweza kufanya jambo lolote lile na jinsia yao si kikwazo.

Ila, mambo kama haya kwa mtu kama Makonda, ni mambo makubwa sana yaliyomzidi kimo.

Ndo maana anaona kumkata mwanaume asilimia 40 ya kipato chake kama ndo suluhisho 🤣.

The guy is dangerously stupid.

Picture him being president in an imperial presidency like the one we have now...

He could rule by diktat on a whim almost every single day.
 
Lawama kwa Kikwete na Magufuli aliyemteua na anayeendelea kumuacha.

Lakini naona Magufuli naye haoni tatizo, kwa sababu wote hawajapishana kitu.
 
Aibu ya kung'azishwa na bawacha... Anataka ajisafishe aonekane alikuwa na nia nzuri.
 
Niliiona hii kwenye kituo cha mwendokasi.
 
Huyu Makonda ana ajenda gani na wanawake? kila siku wanawake wanawake kama anawahurumia na anatakakuwasaidia kweli,siaitake serekali yake iwalipe wanawake hizo asilimia 40 kupitia kwenye mshahara wa waume zao kuliko kutoa matamko ambayo hayawezekani wakati mshahara wenyewe hata nusu mwezi hautoshi.
 
Amekuwa bunge kupitisha hiyo sheria au anabwabwaja ovyo kama kawaida yake. This man ooh, tuzidi kumhurumia tu!!!
 
Hivi anaijua mentality ya mwanamke? akipewa hiyo 40% bado ataikodolea macho ile uliyobaki nayo ifanye matumizi yote ya nyumbani pamoja na nywele zake na kucha, hiyo 40% inakoishia haijulikani..
 
Hili jamii daima huwa linaibua vitu minor, na vyote halivikamilishi.Kwa kufikiria kipuuzi,linadhalilisha u RC!Kwa kukirupuka hv,inafaa litumbuliwe, cjui uncle huwa analilea kwa nn yan!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…