Makonda: Wanaume wafanyakazi wakatwe asilimia 40 ya mishahara yao wapewe wake zao

Makonda: Wanaume wafanyakazi wakatwe asilimia 40 ya mishahara yao wapewe wake zao

Fungu la kumi 10%
Wife alowance 40%
SSF 10%
PAYE 11%
Loan board 15%
Staff loan 25%
Health insirance 05%

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji38][emoji23][emoji38][emoji38] home unarudi na mjogojo unaning'inia ndani ya boxer khaaaaaaaah, nyie wanaume mumuombe msamaha PAUL uwiiiiiiiiih

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi wangu nampaga 100% za mshahara. Kwa maana hiyo namuachia ATM card yangu.
Kwa sharti kuwa asiniulize chochote kuhusu chakula, kusomesha, matibabu, mavazi na kunitunza mimi kwa yote hayo.
Anachoshangaa anaona nadunda siombi hela kwake na simuombi hela ya mafuta ya gari wala za bar.
Kuna mahali anatamani anirudishie kadi yangu nipange mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi wangu nampaga 100% za mshahara. Kwa maana hiyo namuachia ATM card yangu.
Kwa sharti kuwa asiniulize chochote kuhusu chakula, kusomesha, matibabu, mavazi na kunitunza mimi kwa yote hayo.
Anachoshangaa anaona nadunda siombi hela kwake na simuombi hela ya mafuta ya gari wala za bar.
Kuna mahali anatamani anirudishie kadi yangu nipange mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaakiri sana wewe jamaa,kweli mchawi mpe mwanao akulelee.hapo shemeji anatamani kuomba poo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio mkuu maana hii Sharia inaubaguzi sana itafanya tusio na ajira tutakosa wanawake bhana
Sasa mkuu, wamesema wanataka wawe wanakata 40% ya kiasi cha mishahara ya hao wanaotumika, sasa utakuwa unakatwaje ? au utakuwa unapeleka mwenyewe ?, pia ni lazima tujue mapato yako kwa mwezi
 
Mimi wangu nampaga 100% za mshahara. Kwa maana hiyo namuachia ATM card yangu.
Kwa sharti kuwa asiniulize chochote kuhusu chakula, kusomesha, matibabu, mavazi na kunitunza mimi kwa yote hayo.
Anachoshangaa anaona nadunda siombi hela kwake na simuombi hela ya mafuta ya gari wala za bar.
Kuna mahali anatamani anirudishie kadi yangu nipange mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usije kuwa unawa attract wale CID waanze kukufuatilia Mkuu !!
 
Dada zetu wengine hawana shida ya pesa. Shida yao ni kutojiamini na kujiona wamepigwa pasi au hawana tako.
RC aliangalie hili ili wanaume waliojaliwa mitako, angalau wapunguze kwa asilimia 40 na kuwapa dada zetu wenye uhitaji.

Imekaaje hii wakuu?
 
Sasa mkuu, wamesema wanataka wawe wanakata 40% ya kiasi cha mishahara ya hao wanaotumika, sasa utakuwa unakatwaje ? au utakuwa unapeleka mwenyewe ?, pia ni lazima tujue mapato yako kwa mwezi
Inategemea na dili limejiseti vipi
 
Sina mengi saaana nitaandika kwa Kifupi ikisapotiwa na picha. #tafadhali RC jiji letu KAMUULIZE RAHEEM STERLING ugumu wakazi aliyoifanya alafu KUKATWA 40%
Rejea na picha
IMG_20200311_041706_122.jpeg
IMG_20200311_041706_129.jpeg
images%20(36).jpeg
images%20(34).jpeg
images%20(35).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attachments

  • IMG_20200311_041706_127.jpeg
    IMG_20200311_041706_127.jpeg
    18.2 KB · Views: 1
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema anatarajia kupeleka muswada binafsi bungeni, kutaka itungwe sheria ambayo itamka mwanamume ambaye ni mfanyakazi, kukatwa asilimia 40 kwa ajili ya mke wake ambaye ni mama wa nyumbani.

Makonda alisema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika kimkoa kwenye Viwanja vya Leaders wilayani Kinondoni.

Makonda alisisitiza kuwa hataki kumwona mwanamke yeyote katika Mkoa wa Dar es Salaam akinyanyasika, ndio maana aliamua kuwasaidia wanawake waliotelekezwa na wenza wao na kutoa namba 0682009009 ambayo wanaweza kupiga bure.

Alisema baada ya kuona tatizo lilivyo kubwa la wanawake, ambao wanadhulumiwa mali za wenzao wao baada ya kufariki, kamati iliyokuwa ikisikiliza wajane hao iliandika mapendekezo sheria ya mirathi na imekabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

“Baada ya kamati niliyounda kusikiliza madai ya mirathi tulikuta tatizo ni kubwa, hivyo tuliandika taarifa tukamkabidhi Ummy Mwalimu pia tukaomba sheria ya mirathi itamke kuwa endapo baba atatangulia mbele ya haki basi mama awe ndio msimamizi wa mirathi,” amesema Makonda.

Alisema Sheria ya Ndoa ya Tanzania, imerithiwa kutoka India na ina zaidi ya miaka 120, hivyo sheria ikimpa haki mama lazima atampa mali mwanawe, si kama baba wadogo au shangazi wanavyokuwa wasimamizi wanavyofanya mali hizo kuwanufaisha wao na familia zao na kuwaacha walengwa wakitaabika.

Makonda pia aliwataka wanawake kuwa walezi wazuri wa watoto wao, hata kama wametekelezwa, kuliko kuwajaza maneno yenye uchungu waliokutana nao baada ya kutelekezwa, kwani kufanya hivyo kunasababisha kuwa na kizazi kisichokuwa na maadili.

“Mama unamtolea mtoto wako maneno yenye uchungu baada ya kutelekezwa na baba yake, huyo mtoto haimuhusu kwani kila wakati mnakutana hakuwepo hivyo pambana na hali yako maana tunawafanya watoto waone maisha ndio yalivyo, wengine wanakataa kuolewa wakidhani wanaume wote wako hivyo,” alisema.

“Televisheni zimeleta malezi mengine kwa watoto wetu bila hata kwenda nje ya nchi wameiga tabia ambazo ni kinyume na maadili yetu hivyo wazazi jengeni tabia ya kuzungumza na watoto wenu na kufuatilia mwenendo wake, usingoje kujua tabia za mwanao kutoka kwa dada wa kazi au jirani,” aliongeza.

Alisema wanawake wanatakiwa kupambana na utamaduni wa makabila unaokataza wanawake kurithi mali, mfumo dume na kuishi kwa kusubiri kuambiwa unaweza bali mwanamke ajikubali kuwa anaweza bila kuambiwa na mtu.

Aliwataka wanawake kujiimarisha kiuchumi kwani akiwa na kipato hatonyanyasika, na kueleza kuwa katika kila halmashauri kuna mikopo isiyo na riba wanayoweza kukopa na kwa mwaka jana hadi sasa zaidi ya Sh bilioni 40 vimekopeshwa.

Kila mwaka Machi 8 ni Siku ya Wanawake Duniani na ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana jijini New York nchini Marekani, wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura.

Mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake jijini Copenhagen nchini Denmark walikubaliana kwa pamoja na mara ya kwanza ilisherekewa mwaka 1911, Austria, Denmark, Ujerumani na Uswisi. Sherehe ya 100 ilifanyika mwaka 2011, hivyo mwaka huu ni sherehe ya 107 ya wanawake duniani na kitaifa imefanyika mkoani Simiyu ambako mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
View attachment 1381780
Chanzo: HabariLeo
IQ ya Bashite iko chini mno huku anapinga uchoko lakini matendo yake ni ya kichoko zaidi ya machoko na ulaya walianza hivi hivi baadae wakajitangaza na kutaka kuolewa kabisa. Kichwa chake hakifikiri zaidi ya anayosema.
 
Akili na Elimu ni vitu Viwili tofauti kabisa
Kwa maana havina uhusiano unaweza ukawa na Elimu ukakosa Akili,vivyo hivyo
Unanaweza ukawa na Akili lakini Elimu huna binafsi huwa siangalii Elimu mi naangalia AKILI mtu mwenye uwezo wa kutafakari mambo ya busara sio blaablaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom